Posts

Fahamu Kwa nini Unapaswa Kujenga Tabia ya Kujisomea Vitabu (Faida za Kujisomea Vitabu)

Image
(Sehemu ya Pili) Habari... Mara ya mwisho tuliangazia sehemu ya kwanza ya somo hili ambapo tuliangalia kwa utondoti sababu za kwa nini watu hawapendi/hawana utamaduni wa kujisomea vitabu. Moja ya sababu ambayo tuliangalia ni watu kutojua umuhimu wa kujisomea vitabu.   Basi leo katika sehemu hii natamani tujue faida za kusoma vitabu pengine tunaweza kuwaamsha baadhi ya wenzetu na kuwatia hamu ya kusoma. Zifuatazo ni faida za kujisomea vitabu; >> Kuongeza Maarifa: Vitabu ni chanzo kikuu cha maarifa na taarifa. Kusoma vitabu kunakuwezesha kujifunza mambo mapya na kuongeza uelewa wako wa ulimwengu. >> Kuboresha Uwezo wa Kufikiria: Kusoma vitabu kunachochea ubongo kufanya kazi, hivyo kuboresha uwezo wako wa kufikiria kwa undani, kutatua matatizo, na kufanya maamuzi bora. >> Kuboresha Lugha na Msamiati: Kusoma vitabu husaidia kuboresha uwezo wa lugha, kuongeza msamiati, na kuelewa matumizi sahihi ya maneno. >> Kuongeza Uwezo wa Kujieleza: Kusoma vitabu kunasaidia ...

KWA NINI WATU WENGI HAWANA UTAMADUNI WA KUJISOMEA VITABU?

Image
 Kwa Nini Watu Wengi Hawana Utamaduni/Hawapendi Kujisomea Vitabu?  (Sehemu ya Kwanza) Habari... Siku kadhaa zilizopita niliandika kwenye kurasa zangu za mitandao ya kijamii mara baada ya kufanya kipindi cha 'The Fix' cha redio kuhusiana na mada inayosema 'Kwa Nini Watu Wengi Hawapendi Kusoma Vitabu?' Nakumbuka baada ya chapisho lile niliahidi kukufikishia somo lote hatua kwa hatu. Sasa leo natamani somo hili liwe kama sehemu ya kwanza na mada ile ile ambapo leo tutaangalia sababu za watu wengi kutokuwa na mwamko, shauku ama utamaduni wa kujisomea vitabu. Zifuatazo ni baadhi tu ya sababu za watu wengi kutokuwa na utamaduni wa kujisomea vitabu; >> Mabadiliko ya Teknolojia (Simu na Mitandao ya Kijamii); Vifaa vya kisasa kama simu za mkononi, kompyuta, na mitandao ya kijamii vimechukua nafasi kubwa katika maisha ya watu. Watu wengi wanapendelea kutumia muda wao kwenye mitandao badala ya kusoma vitabu. >> Video na Habari za Papo kwa Papo; Watu wanaweza kupata hab...

Mbwa Bado Hajafa! (Usikubali Kukata Tamaa)

Image
Meshack Siwingwa 0764 987 588 Jamaa mmoja alikuwa akisafiri kutoka nyumbani kwake kuelekea mjini majira ya saa moja asubuhi. Baada ya mwendo wa kama saa mbili hivi alikutana na kijana mmoja akiwa amesimama barabarani akingojea kumwona mtu aendaye mjini ili aweze kumuomba 'lift.' Kijana huyu alikuwa amebeba vifaa kadhaa vinavyotumika kwa ajili ya usafi wa kuoshea magari vile ambavyo alivimudu kuvibeba. Kando ya huyu kijana alikuwa amelala mbwa aliyeonekana kuwa dhooofu bin hal kwani alikuwa akitweta kwa uchungu uliosababishwa na maumivu aliyokuwa nayo. Yule kijana alipunga mkono kwa jamaa ndipo jamaa aliposimamisha gari yake na kuamua kumsikiliza kijana. Kijana alimweleza jamaa kwamba alikuwa anaelekea mjini kumtibia mbwa wake na kwamba baadhi ya vifaa kadha alivyokuwa navyo alitegemea apate kazi za kuosha magari pindi afikapo mjini ili aweze kupata fedha za kumudu gharama za matibabu ya mbwa wake. Jamaa alishangaa sana baada ya kuona hali ya mbwa wa yule kijana na ndipo alipoam...

SABABU KUBWA (06) KWA NINI WAFANYABIASHARA 'WANAOJITAMBUA' WANATUMIA BUSINESS CARDS

Image
 Yes, unaweza kuonekana ni mtindo mgeni wa maisha lakini hii ni moja kati ya njia rahisi sana za kufanya marketing ya biashara au huduma yako. Matumizi ya business cards katika kutangaza biashara au huduma yako yana faida kadhaa kubwa sana.  Hapa chini ni faida chache tu! Mosi, business cards huonesha smartness kwenye ufanyaji wa biashara au utoaji wa huduma yako. Mtu yeyote yule anapokuomba mawasiliano yako ukampatia business cards; moja kwa moja anajua kwamba upo serious na unajua vyema unachokifanya. Pili, business cards hujenga uaminifu. Wateja wengi hukuamini wewe pamoja na huduma au biashara yako hasa mara baada ya kujiridhisha kwamba uko formal sana.  Tatu, huongeza ujasiri. Unapotumia business cards kuendesha huduma au biashara yako, hii inakuongezea ujasiri hata wewe mwenyewe hasa pale ambapo mtu anakuomba contacts unampatia business cards 😎 Nne, ni njia mojawapo ya kutangaza biashara au huduma unayofanya. Tuchukulie mfano umekutana na ndugu ambaye muda mrefu ha...

Je, Huyu ni Wewe?

Image
Je, unahitaji kudesign na kuprinti stickers? Je, unahitaji kudesign na kuprinti vitabu vya tickets? Je, unahitaji kudesign na kuprinti ID Cards? Je, unahitaji kuprinti t-shirts? Je, unahitaji kudesign na kuprinti vitabu vya risiti (receipt books)? Je, unahitaji kudesign na kuprinti flyers? Je, unahitaji kudesign na kuprinti business cards? Je, unahitaji kudesign na kuprinti vitabu vya malipo (payment vouchers)? Wala Usipate Shida... ... Msomi Huru Enterprises Co. LTD ndiyo jibu lako! Tunafanya designing za ubora wa hali ya juu pamoja na printing aina zote (zenye viwango vya TBS) Tunakukaribisha sana kufanya kazi na sisi na kwa hakika, HAUTAJUTA KUTUAMINI📌 Wasiliana nasi kwa simu namba: 0764 987 588 Barua pepe:  msomihurugroup@gmail.com Tupo Mzumbe - Morogoro Karibuni Sana!

HIZI HAPA SABABU 100+ KWA NINI UNATAKIWA UKUZE BRAND YAKO KWANZA NDIPOSA UONE MAFANIKIO YAKITIRIRIKA KAMA MAJI YA MTO YORDANI!

Image
  Watu wengi sana ambao ni wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali huwa wanajikuta wakiwa kwenye mkanganyiko mkubwa mkubwa sana wa kipi wanachotakiwa kufanya kati ya kukuza brand zao kwanza ama kuendelea kutoa huduma tu. Wengine hukaribia hata kiasi cha kukata tamaa hasa pale wanapokuwa hawaoni matokeo ya kile wanachokifanya. Ukweli ni kwamba, ni muhimu sana kukuza brand yako wakati unaendelea kutoa huduma ama kufanya biashara zako ili watu waweze kukuamini na kufanya kazi na wewe ama kununua kutoka kwako. Hii inasaidia kiasi kwamba unafika wakati ambapo wateja wakiwa na uhitaji mbalimbali lazima waje kununua kutoka kwako kwa sababu ya brand yako. Wakati mwingine kinachokusaidia kuuza au kupata wadau siyo aina ya bidhaa zako unazotoa, bali ni kwa sababu ya brand au jina lako linavyofahamika. Habari njema ni kwamba, hata wewe unayonafasi kubwa sana ya kupambania brand yako wakati unaendelea kufanya biashara yako. Brand itakutangaza na kukufanya uaminike.  Unaweza kuamua sasa...

JINSI YA KUTENGENEZA BRAND IMARA

Image
Kila mtu anaweza kutengeneza BRAND imara kwa ajili ya taasisi, kampuni ama kikundi chake kwa kufanya yafuatayo:- 1. Sajili taasisi, kikundi, kampuni au biashara yako ili itambulike kisheria. 2. Tengeneza kanuni ambazo wafanyakazi ama wafuasi wako watazifuata. Kila mtu katika kutekeleza majukumu yake azifuate kanuni hizo. 3. Fanya kila linalowezekana kampuni, taasisi ama kikundi chako kiwe na uwezo wa kujiendesha hata usipokuwepo. Ukiona kikundi , kampuni ama taasisi yako bado haiwezi kujiendesha usipokuwepo jua kabisa hapo badooooo sanaaaa! 4. Tengeneza Logo, chapa t-shirts ili kutengeneza utambulisho wako kwa watu wanaokuzunguka.  Hii itasaidia watu kufahamu kikundi, kampuni ama taasisi yako pasipo kutumia nguvu kubwa. Sasa basi... Katika kufanikisha haya yoteeee..... Msomi Huru Enterprises Co. LTD inakusaidia kutengeneza brand imara sana kwa; ❇️ Kutengeneza logo, posters ama banners. ❇️ Kusajili kikundi, taasisi ama kampuni yako kwa gharama Nafuu sana (Kuna OFA ya msimu wa sikuku...

15 QUOTABLE QUOTES FROM THE BOOK 'PERMANENT SOLUTION TO YOUTH UNEMPLOYMENT'

Image
Author; Dr. Abib Olamitoye Analyst; Mr. Mashaka Siwingwa (CEO Msomi Huru Foundation) +255 764 987 588 01. "Do as I do is always better than do as I say." (Page 7-8) 02. "Whatever any man can accomplish, every other man also carries the capacity to do just as well." (Page 8) 03. "The stomach needs good food and the brain needs good books, for the man to function maximally." (Page 10) 04. "To make most of his God given potential, to exploit his talents to the peak, a man needs to feed the body daily and feed the brain daily." (Page 10) 05. "One of the fruits of the skill of saving is patience. You get to establish that the best way to get rich is to get rich slowly, and this is also the surest way to become rich with peace of mind." (Page 14) 06. "When the time to begin the business has come, the time to save up the capital has passed." (Page 15) 07. "There are basically two reasons why we set up a business, namely, to crea...

HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUJIEPUSHA NA MAMBO YASIYOFAA

Kwenye maisha tunaishi na watu tofauti tofauti na wenye mitazamo tofauti tofauti. Watu hao huweza kuwa na mitazamo mizuri ama mibaya juu ya mambo fulani. Mathalani, hata wewe kuna baadhi ya mambo ukiyaona unaweza kuyapambanua kama ni mazuri au mabaya. Wakati mwingine hutakiwi hata kusubiri kuambiwa kama jambo hilo ni jema ama baya. Ni mara nyingi sana (kama siyo zote) kwa marafiki hupeana au kupashana habari au taarifa fulani. Taarifa au habari hizo huhusu mambo yanayozizunguka jamii hizo. Wakati mwingine marafiki huweza kusambaza habari hizo na kutuletea bila kuzipima kwa kina na kuweza kuzichuja ili kujua kama zinafaa au la! Na wakati mwingine habari hizo huwa hazifai kabisa kusambazwa! Kosa letu kubwa ni pale ambapo tunaamua kusambaza taarifa au habari ambazo tumezipokea tu kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki zetu bila kuweza kuzipima wala kuzichuja ili kuweza kujua uhalali wa habari hizo. Ikiwa tumepokea taarifa au habari zisizoaminika kutoka kwa marafiki zetu moja kwa moja tunaten...

SIFA KUU YA MTU MWONGO

Ukiwa mtu mwongo ni raha sana kwa sababu ukidanganya mara ya kwanza utatamani udanganye tena na tena. Uongo ni mtamu kuliko ukweli na ni rahisi kuusema kwa sababu unavutia na kufariji kwa muda mfupi. Muhimu tu ni kwamba ukiwa mwongo unatakiwa baada ya kudanganya mara ya kwanza, ya pili na ya tatu uwe na kumbukumbu, ukumbuke mara zote ulizodanganya tena kwa mpangilio ule ule. Zaidi, uwe na uwezo wa kuwakumbuka uliowadanganya; hapo ndipo unapokuja kukamatwa kwa sababu uongo hauna sifa ya kudumu.  Watu hujisahau mara tu baada ya kudanganya na huwa hawana uwezo wa kukumbuka tena. Ndiyo maana hata kwenye sheria (mahakamani) watu hukamatwa na hatia mara baada ya kuchanganya maelezo ya awali na yale yaliyofuatia. Unakuta mtu baada ya kueleza sentensi A anashindwa kuiunganisha na sentensi B na C kwa sababu sentensi A haikuwa na ukweli. Hivyo, anakuwa na uwezekano mkubwa wa kuchanganya mambo na kukutwa na hatia. Ndugu yangu, ukweli unahitaji vithibitisho vingi na vielelezo vingi ili kuweza ...

HIVI NDIVYO TUNAVYOWEZA KUSAPOTI WAHITIMU WAPYA KUANZISHA BIASHARA

Na:- Mashaka Siwingwa +255764987588 ____________________________________________________________________________________ Mnamo Juni 2021, niliweza kupokea kadi za aina tatu tofauti tofauti. Ninaweza kusema kwamba ulikuwa ni mwezi wa neema sana kwangu kiasi kwamba nilithaminiwa mpaka kufikia hatua ya kupewa kadi. Kadi ya kwanza ilikuwa imenakshiwa safi kabisa kwa rangi ya mzambarau. Ilikuwa ni kadi nzuri na yenye kuvuti. Ilikuwa ni kadi iliyoambatanishwa na jina langu kabisa tena kwa herufi kubwa. Baada ya kuifungua na kuisoma ilikuwa ikinitaka kuchangia harusi ya rafiki yangu ambaye alitarajia kufunga pingu za maisha Oktoba, 2021. Nilimshukuru sana Mungu kwa kitendo cha mimi kuonekana wa maana mpaka kufikia hatua ya kupewa kadi ya kuchangia harusi. Hiyo niliiweka chini. Baada ya kuiweka chini niliichukua kadi ya pili. Hii ilionekana kuwa ya hadhi ya chini kidogo na haikupambwa sana kama ile ya awali. Niliipokea kutoka kwa rafiki yangu wa karibu. Nilivyoifungua na kuisoma niligundua kwa...

TOFAUTI KUBWA ILIYOPO KATI YA UONGOZI NA CHEO

Mara nyingi watu huchanganya kati ya hizi dhana mbili. Watu wengi hudhani kwamba ziko sawa na wachache hudhani kwamba zinatofautiana. Ndiyo! Inawezekana zipo sawa au zinatofautiana kulingana na namna unavyozitafsiri dhana hizi.  Siku ya leo ninaomba niwasaidie wale wanaojua dhana hizi zinaendana 100% na hawawezi kabisa kutofautisha kati ya dhana hizi. Uongozi ni madaraka anayopewa mtu ya kusimamia au kuongoza. Au ni majukumu ambayo mtu hukabidhiwa ili ayatekeleze. Kwa upande mwingine tuna istilahi 'Cheo.' Istilahi hii ina maana nyingi kwa mujibu wa waandishi mbalimbali na kamusi mbalimbali za lugha ya kiswahili. Kwa mujibu wa kamusi moja inasema 'Cheo' ni nafasi ya hadhi ambayo mtu anapewa kazini. Lakini pia kuna maana isemayo 'Cheo' ni ubao utumikao kusukia ukili. Zaidi ni kwamba kuna tafsiri nyingi sana na nyingine ni tofauti sana na lengo letu. Sasa lengo letu ni kutofautisha dhana ya cheo kama hadhi ya heshima anayopewa mtu na uongozi kama dhamana ya majukum...

UKITAKA WATU WAKUHESHIMU FANYA HIVI

Kila mtu anastahili kupewa heshima na kuthaminiwa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba heshima na thamani ni kitu ambacho kila mtu anastahili. Haijalishi elimu zetu, tamaduni zetu, makabila yetu, dini zetu wala maeneo tunayotokea. Kutokuheshimiana ni moja ya kitu ambacho kimekuwa kikisababisha migogoro kwa watu mbalimbali. Mtu mmoja anaposhindwa kumheshimu mwenzake hupelekea migogoro na hata kuvunja ukaribu wao. Marafiki wawili wanaposhindwa kuheshimiana huwa hawana haja tena ya kuona kama urafiki wao una manufaa yoyote yale bali huamua kuvunja urafiki wao. Wapenzi wengi pia wanaposhindwa kuheshimiana hupelekea mogogoro kwenye mapenzi yao na hata kuvunja mahusiano. Mathalani, wanandoa wanaposhindwa kuheshimiana na kuthaminiana hupelekea  migogoro ndani ya nyumba na hatimaye kuamua kuvunja mahusiano au ndoa yao. Kwa kawaida, suala la kutoheshimiana ni suala la mtu mmoja mmoja kwani ni matokeo ya ubinafsi baina yetu. Kwa mujibu wa Dkt. Issaya Lupogo & Aziza Lupogo (2019) katika kita...

SAA ZA KIBONGO DHIDI YA SAA ZA KIZUNGU: WABONGO TUNAZINGUA SANA

Na: Mashaka Siwingwa __________________________________________ "Do you love life? Then do not squander time; for it is the stuff that life is made of." Ilikuwa ni kauli ya Benjamin Franklin kama alivyonukuliwa na Brian Tracy katika kitabu chake cha Time Power. Siku hizi wabongo tumetumbukia katika balaa; naam balaa zito kwelikweli. Balaa la kushindwa kuwa na nidhamu; nidhamu katika matumizi ya muda. Siku hizi kuna muda wa kibongo na muda wa kizungu. Mtu akikwambia tukutane saa saba kamili saa za kibongo basi ujue hiyo ni saa tisa kama siyo saa kumi na nusu. Mtu akikwambia tukutane saa nane kamili saa za kizungu basi ujue hiyo ni saa nane kamili kama ilivyotajwa. Hizi kauli za "saa za kibongo"  na "saa za kizungu"  tumezitengeneza wenyewe aidha kwa kujua au kutokujua. Tumekuwa tukiwaabudu wazungu bila kujua kwa sababu tunakubali kila kilicho cha kwao.   Saa za kibongo ni ishara ya dharau na kukosa uaminifu wakati saa za kizungu ni uaminifu na "commitm...

"MUUZA KIFO AFARIKI DUNIA"

Kaka wa mtengeneza silaha maarufu duniani, Alfred Nobel alifariki dunia na waandishi wa habari wakaibuka na kuandika, "Muuza Kifo Afariki Dunia"  Awali, waandishi wa habari waliamini kwamba aliyefariki ni Alfred Nobel ambaye alikuwa ni mtengeneza mabomu na silaha za moto kwa kutumia madini ya dainamaiti. Alfred Nobel alikuwa mtengenezaji mabomu wa dainamaiti na alifanya kazi hiyo kama sehemu yake ya kujiingizia kipato. Ulimwengu ulimchukia kwa sababu aliuza kifo na kwa bahati mbaya hakufanikiwa kung'amua kitu cha namna hii.  Alfred Nobel aliishi maisha ya furaha sana kwa kuwa na kipato kizuri kupitia kuuza silaha hizo hatari. Kwa bahati mbaya ni kwamba hakufanikiwa kujua namna ambavyo alikuwa anachukiwa na jamii yake kwa kazi hiyo haramu. Baada ya miaka kadhaa kupita, kaka yake alifariki na waandishi wa habari baada ya kupata habari hizo wakajua aliyefariki ni Alfred aliyekuwa akitegemea kazi ya kutengeneza mabomu na silaha kama sehemu yake ya kujiingizia kipato. Waandish...

KAULI KUMI ZA HAYATI MWL. JULIUS K. NYERERE KUHUSU ELIMU NDANI NA NJE YA NCHI

Na; Mashaka Siwingwa +255764987588 ----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------- Ni miaka mingi imepita tangu atutoke baba wa taifa Hayati, Julius Kambarage Nyerere. Ushujaa na uhodari wake katika kupambanua mambo pamoja na kueleza vitu bayana kunamfanya aendelee kuwa shujaa asiyesahaulika. Wakati wa uhai wake, baba wa taifa alisisitiza sana juu ya suala la elimu hapa nchini. Falsafa yake ya kuamini kwamba elimu ndiyo silaha pekee ya kuufikia ukombozi wa kweli hasa kifikra. Katika nyakati tofauti tofauti, katika sehemu tofauti na katika muktadha tofauti, Hayati baba wa taifa aliweza kuonesha wazi msimamo wake juu ya mfumo wetu wa elimu. Kati ya mengi aliyoyazungumza, leo nimeamua nikukusanyie kauli kumi tu alizowahi kuzitoa shujaa huyu.  Twende sawa; 1. Kauli aliyoitamka mnamo tarehe 31 Desemba, 1969 akizungumza na vyombo vya habari kuhusu malengo ya Elimu ya Watu Wazima. Alisema, "... education is som...

TABIA KUMI RAHISI SANA ZA KUFANYA ILI UANZE KUFANIKIWA

Na; Mashaka Siwingwa +255764987588 ----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------- Suala la kufanikiwa siyo tukio la sekunde moja au siku moja kama wengi wadhanivyo. Ni mchakato mrefu na wenye mfululizo wa matukio kadhaa. Hata hivyo, tulio wengi hatujui kanuni bora za kupitia ili tuweze kufanikiwa. Kwa kubeza ujumbe huu, kuna mdau anayeniona kila siku atasema mbona mimi sijafanikiwa! Shauri yako.  Ili uweze kufanikiwa unahitaji vitu kadhaa muhimu sana. Hivi vitu vitaamua hatma ya maisha yako katika nyanja mbalimbali.  Pasi na shaka, kuna mtu ataauliza kama kuna nyanja za maisha. Ndiyo, kuna nyanja mbalimbali za maisha. Kati ya hizo ni pamoja na kufanikiwa kiuchumi, kijamii, kisiasa, kiutamaduni na kadharika. Baadhi ya tabia zifuatazo zinaweza kumtengenezea mtu mazingira ya kufanikiwa moja kwa moja. Au zinaweza kuwa mwanga wa mafanikio yake. Kanuni au tabia hizo ni pamoja na; 1. Mtu anayezingatia kanu...

KUJUA SIYO KUTENDA, TUJITATHIMINI

Na; Mashaka J. Siwingwa +255764987588 ----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------- Ukienda kanisa lolote lile lazima utakutana na watu wa aina tatu. Wale walio moto kwenye masuala ya kikanisa, wale ambao ni vuguvugu na wale ambao ni baridi kabisa.  Watu ambao wako moto kwenye masuala ya kikanisa, wao hushiriki katika kila shughuli ya pamoja, huweza kuhamasisha na kuwatia moyo wengine ili waweze kushiriki pia, hawa hawakati tamaa na ni waaminifu sana kwenye masuala ya kiimani japokuwa kuna changamoto za kiubinadamu pia. Mara nyingi hawa huwa ni viongozi. Watu ambao ni vuguvugu, wao husubiria hamasa kwenye kila jambo ili waweze kushiriki katika shughuli fulani. Wao husubiri watengenezewe mazingira ya urahisi au ugumu wa jambo fulani ndipo waamue kama waliunge mkono au walipige kipepsi. Hawa watu mara nyingi wanahoji sana. Kwa mfano, kiongozi yeyote yule wa kanisa anapotangaza maombi ya mfungo wa wiki m...

MIMEA HUHITAJI MIZIZI ILI KUKUA; BINADAMU TUNAHITAJI WATU ILI KUFANIKIWA

Na; Mashaka J. Siwingwa     +255764987588 ___________________________________________________________________________________ Ili mimea iweze kuota, kukua na kustawi vizuri inahitaji mizizi imara na yenye uwezo wa kustahimili ukame wakati wa dhiki. Mizizi huisaidia mimea kuweza kufyonza maji katika umbali mrefu hatimaye kuusaidia mmea kuendelea kuishi. Kustawi kwa majani na matawi ya miti ni matokeo ya kazi ngumu inayofanywa na mizizi ambayo hata hivyo siyo rahisi kuiona, kwa sababu hupatikana ardhini. Mizizi haihitaji kujionesha ili kufanya kazi ya kufyonza maji na kuyasaidia majani kustawi. Wakati mwingine ni kwamba, mizizi inapata shida sana kutafuta maji katika umbali mrefu hasa wakati wa ukame. Naam... mizizi hustahimili dhiki zote hizo. Binadamu na wanyama wengine wapitapo kando ya mimea hiyo hufurahia kuiona ikiwa imestawi vizuri bila kujua kama kuna kitu kinaitwa mizizi kinafanya kazi chini kwa chini. Mizizi haihitaji shukrani ya binadamu wanaopata kivuli ili kuendelea...

KAULI YA "LETA KAMA TULIVYO" INAVYOLIGHARIMU TAIFA LETU

Na; Mashaka J. Siwingwa +255764987588 ----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------- Ninajua unaweza kucheka baada ya kusoma kichwa cha andiko hili. Ni kweli, kinaweza kuwa kinachekesha lakini hebu kunywa maji kidogo halafu tuendelee. "Lete kama Tulivyo" ni kauli ambayo imezoeleka na kuwa ya kawaida sana kwenye taifa letu. Sijajua kama na mataifa mengine yanaathiriwa na vitu vya ajabu namna hii lakini ngoja tujielimishe sisi wenyewe kwanza. Kauli hii imekuwa ikitumiwa sana na watu wa rika moja, wenye mambo yanayoendana, wenye elimu zinazoendana tena ambao kwa namna moja ama nyingine wanakuwa ni marafiki wa karibu sana. Tatizo si wao kuwa na umri sawa, kuwa na kiwango sawa cha elimu wala kuwa marafiki wa karibu sana. Shida ni muktadha ambao kauli hii imekuwa ikitumika. Kuna rafiki yangu mmoja nilisoma naye shule moja. Siku moja akawa ananisimulia kuhusu mzazi wake. Kwamba mzazi wake alikuwa anasumb...