"MUUZA KIFO AFARIKI DUNIA"


Kaka wa mtengeneza silaha maarufu duniani, Alfred Nobel alifariki dunia na waandishi wa habari wakaibuka na kuandika, "Muuza Kifo Afariki Dunia" 

Awali, waandishi wa habari waliamini kwamba aliyefariki ni Alfred Nobel ambaye alikuwa ni mtengeneza mabomu na silaha za moto kwa kutumia madini ya dainamaiti.

Alfred Nobel alikuwa mtengenezaji mabomu wa dainamaiti na alifanya kazi hiyo kama sehemu yake ya kujiingizia kipato. Ulimwengu ulimchukia kwa sababu aliuza kifo na kwa bahati mbaya hakufanikiwa kung'amua kitu cha namna hii. 

Alfred Nobel aliishi maisha ya furaha sana kwa kuwa na kipato kizuri kupitia kuuza silaha hizo hatari. Kwa bahati mbaya ni kwamba hakufanikiwa kujua namna ambavyo alikuwa anachukiwa na jamii yake kwa kazi hiyo haramu.

Baada ya miaka kadhaa kupita, kaka yake alifariki na waandishi wa habari baada ya kupata habari hizo wakajua aliyefariki ni Alfred aliyekuwa akitegemea kazi ya kutengeneza mabomu na silaha kama sehemu yake ya kujiingizia kipato. Waandishi wa habari baada ya kupata habari hizo haraka wakaandika mara moja, "Muuza Kifo Aaga Dunia." Habari hizi zilimfikia Alfred Nobel na kuzipokea kwa masikitiko makubwa sana. Hapo akaamini kwamba kumbe jamii pana sana ilikuwa ikimchukia kwa kazi yake hiyo na kumvalisha gwanda lenye jina chafu la "Muuza Kifo"

Mara moja akaamua kuachana na kazi hiyo na kuanzisha tuzo ya amani ya "Nobel" ambayo mpaka leo inamtambulisha kila sehemu. Tuzo ya "Nobel" hutolewa kwa mtu mmoja duniani kila mwaka ikiwa na maana ya mwana-amani wa dunia. Historia ya Alfred Nobel ikawa inebadilika namna hiyo.

Usiogope, usitishwe na namna watu walivyokukariri. Kumbe una nafasi kubwa sana ya kubadilika kama utaamua kuchukua hatua na kufanya maamuzi hayo.

Wakati mwingine unaweza kukuta watu wamekukariri kwamba wewe ni mlevi maarufu, mvuta sigara maarufu, mzinzi maarufu, mchawi maarufu, umepewa kila sifa mbaya ambazo wakati mwingine zimekolezwa tu (hustahili sifa hizo). Sasa unayo nafasi ya kubadilisha maisha yako na kuuaminisha ulimwengu kwamba wewe siyo yule wanayemjua siku zote. Unaweza kufanya mapinduzi mpaka kuzimu ikashangaa.

Unao uwezo mkubwa sana wa kuibadilisha lebo chafu ambayo umevalishwa sasa hivi na kuvaa lebo safi ya baraka na mafanikio tele.

Cha msingi ni kuketi chini na kutafakari ni jina gani baya ulilonalo ambalo kimsingi hustahili... Pambana ubadili laana kuwa baraka, jangwa kuwa ziwa, njaa kuwa shibe, umasikini kuwa utajiri, upumbavu kuwa uelewa na dhiki kuwa faraja.

Pambana uanze, anza na moja, piga hatua nyingine, nenda tena, piga hatua zaidi. The world won't change unless you do!

Tough Times Never Last But Tough People Do.

"Njia sahihi ya kusonga mbele ni kuanza kutembea"

Mashaka Siwingwa

Mzumbe University

Comments

Popular posts from this blog

KWA NINI WATU WENGI HAWANA UTAMADUNI WA KUJISOMEA VITABU?

Mbwa Bado Hajafa! (Usikubali Kukata Tamaa)

KAULI KUMI ZA HAYATI MWL. JULIUS K. NYERERE KUHUSU ELIMU NDANI NA NJE YA NCHI