SIFA KUU YA MTU MWONGO

Ukiwa mtu mwongo ni raha sana kwa sababu ukidanganya mara ya kwanza utatamani udanganye tena na tena. Uongo ni mtamu kuliko ukweli na ni rahisi kuusema kwa sababu unavutia na kufariji kwa muda mfupi.

Muhimu tu ni kwamba ukiwa mwongo unatakiwa baada ya kudanganya mara ya kwanza, ya pili na ya tatu uwe na kumbukumbu, ukumbuke mara zote ulizodanganya tena kwa mpangilio ule ule. Zaidi, uwe na uwezo wa kuwakumbuka uliowadanganya; hapo ndipo unapokuja kukamatwa kwa sababu uongo hauna sifa ya kudumu. 

Watu hujisahau mara tu baada ya kudanganya na huwa hawana uwezo wa kukumbuka tena. Ndiyo maana hata kwenye sheria (mahakamani) watu hukamatwa na hatia mara baada ya kuchanganya maelezo ya awali na yale yaliyofuatia. Unakuta mtu baada ya kueleza sentensi A anashindwa kuiunganisha na sentensi B na C kwa sababu sentensi A haikuwa na ukweli. Hivyo, anakuwa na uwezekano mkubwa wa kuchanganya mambo na kukutwa na hatia.

Ndugu yangu, ukweli unahitaji vithibitisho vingi na vielelezo vingi ili kuweza kuaminika lakini uongo mmoja tu huweza kufuta hayo yote. Hauhitaji kulipwa mabilioni ya fedha ili kusema ukweli bali uongo kwa sababu ukweli una sifa ya kujilipa tofauti na uongo.

Amua leo kusema ukweli daima maishani mwako.

(Maandalizi ya kitabu cha Self-Management)

Mashaka Siwingwa

Chuo Kikuu Mzumbe. 

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

KWA NINI WATU WENGI HAWANA UTAMADUNI WA KUJISOMEA VITABU?

Mbwa Bado Hajafa! (Usikubali Kukata Tamaa)

KAULI KUMI ZA HAYATI MWL. JULIUS K. NYERERE KUHUSU ELIMU NDANI NA NJE YA NCHI