JE, UNACHANGAMOTO YA RATIBA ZAKO? (USIPITE BILA KUSOMA HII)
Ukipanga kukutana na mtu muda fulani, muda huo ukifika na haujakutana naye, baadaye ukimtafuta utamsikia akisema "muda umebana ndugu" au "ratiba ngumu sana aisee!" Ratiba zetu zinabana sana... Hii ni kweli kabisa. Pengine hali kama hii huwa inakupata hata wewe! Unajiona kabisa kwamba hauna muda wa kufanya jambo fulani, lakini ukiangalia kwa makini hata huo muda ulionao sasa hivi hakuna kitu cha maana unachokifanya. Hebu fikiria, leo unaamka saa kumi na mbili kamili asubuhi halafu kesho unaamka saa mbili kamili asubuhi, kesho kutwa unaamka saa moja na nusu kisha mtondo unaamka saa kumi na moja kamili asubuhi. Yaani ratiba zako zinakuwa shaghala baghala! Mbaya zaidi ni kwamba siku ambayo unaamka saa mbili kamili asubuhi unakuta ndiyo siku ambayo una shughuli nyingi za kufanya kuliko siku unayoamka saa kumi na moja kamili alfajiri. Tafakari tatizo liko wapi? Ratiba zetu wengi zimekuwa na mkanganyiko sana hasa pale tunaposhindwa kugundua vipaumbele vyetu kwenye rati...