PIGA MOYO KONDE, KISHA SONGA MBELE

Siku zote mambo huwa hayaji kama vile tulivyotegemea. Siyo kwa ubaya, hapana ni katika hali tu ya kuonyesha kwamba majira hubadilika. Mipango pia hushidwa kutimia. 

Akili yako umeiweka katika upande gani?

Je, unakata tamaa moja kwa moja mara baada ya kukataliwa kazi na kampuni fulani? Je, unakata tamaa moja kwa moja mara baada ya kuachwa na mpenzi wako? Je, umekata tamaa moja kwa moja mara baada ya kuanguka kwa biashara yako? 

Siku zote kitu pekee kinachokukatisha tamaa ni ile hali ya kuamini kwamba jambo fulani liko namna hii au ile, jambo hilo linapokuja tofauti wengi hutahamaki na kisha kukata tamaa...

Amini ninakwambia, siyo kila kitu kitakwenda kama ulivyopanga. Wakati mwingine unatakiwa kukubali kwamba kuna sehemu ulikwama, upige moyo konde kisha kusonga mbele. Maisha huwa hayamsubiri mtu anayevunjika moyo! Na siku zote sekunde, dakika na saa hazisimami ili kukusubiri unapokata tamaa. Jipige kifuani kisha sema SIKATI TAMAA TENA! Kumbuka mtangazaji mkubwa sana  wa Clouds Media, Millard Ayo alituma maombi ya kuomba kazi Clouds Media zaidi ya mara tano bila mafanikio. Kamwe hakukubali kukata tamaa, alipiga moyo konde kisha akaendelea kupambana na siku moja waliamini anaweza na wakaamua kumuita mwaka 2010. Mpaka leo hii ni moja ya watangazaji wanaoaminika sana Afrika wakiwa vijana na wanaoweza kutoa taarifa sahihi ndani ya muda sahihi kote ulimwenguni.

 Kwenye kipaji ulichojaliwa na mwenyezi Mungu, hakikisha unakitendea haki pamoja na kutoruhusu kukata tamaa. Siku zote hakuna mafanikio mepesi.

 Tuzidi kupambana ndugu zangu!


@Chief_Editor

#Msomi Huru. 

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

KWA NINI WATU WENGI HAWANA UTAMADUNI WA KUJISOMEA VITABU?

Mbwa Bado Hajafa! (Usikubali Kukata Tamaa)

KAULI KUMI ZA HAYATI MWL. JULIUS K. NYERERE KUHUSU ELIMU NDANI NA NJE YA NCHI