HAUHITAJI ELIMU KUBWA SANA ILI KUFANYA MAGEUZI KWENYE MAISHA YAKO.

________________________________________

Ni ukweli usiopingika kwamba elimu ni muhimu; tena sana hasa katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia. Elimu ndiyo inayokusaidia kutengeneza mifumo ya kujiongezea kipato hasa kwa kutumia maendeleo ya sayansi na teknolojia. Kupitia elimu uliyonayo, unaweza kutumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara yako, kutoa mafunzo yako kwa watu na kuwashirikisha wengine fursa ya kimaisha uliyoweza kuichungulia. Elimu yangu ndiye kiungo mkubwa na aliyebeba dhamana ya mafanikio yako. Zaidi ya elimu, uelewa na ufahamu wako.

Sambamba na hayo yote, ni dhahiri kwamba wakati mwingine mafanikio hayahitaji elimu kubwa sana kama wengi wanavyodhani, japokuwa kuna njia mbalimbali za kusaka mafanikio; elimu kubwa ikiwemo. Hatuwezi kuubeza mchango wa elimu katika mchakato mzima wa kusaka tonge.

Naam, unaweza kujipima mwenyewe kama elimu uliyonayo kwa wakati huu inaweza kukusaidia kuingiza mkono kinywani, la sivyo endelea kupambana! Elimu ifanyike kuwa mkombozi wa fikra zako, ikupevushe fikra changa ulizonazo, ikufungulie dunia na kukuonyesha fursa mbalimbali za kimaisha, ikuangazie mwanga wa namna unavyoweza kumudu mikiki-mikiki na kashikashi nyingi za maisha. Baada ya hapo, jiongeze!

Hauhijati elimu kubwa sana kuweza kujifanyia mageuzi kiuchumi, kisiasa na kijamii, ndivyo ninavyoweza kukwambia.

Bila shaka unamkumbuka mwamba wa mapinduzi matukufu ya Zanzibar, hayati Abeid Aman Karume aliyesimama na siasa za kijamaa kutoka kwa Mao Ze Dong wa China. Mwamba huyu alizaliwa mnamo mwaka 1905 na kuuliwa mnamo tarehe 07/04/1972. Historia inaonyesha kwamba, Hayati Abeid Aman Karume alianza shule ya msingi mnamo mwaka 1909 na baadaye kuhitimu elimu ya shule ya msingi. Historia ya elimu yake inakomea hapo na kuanza kusimulia harakati za kimapinduzi ambapo walifanikiwa kuunganisha vyama viwili na kuzaa chama cha ukombozi wa Zanzibar kilichojulikana kama Afro Shiraz Party mnamo mwaka 1957. Kutokana na dhamira yake ya dhati kabisa ya kuendesha harakati za ukombozi visiwani, Hayati Abeid Aman Karume alifanikiwa kuwa Rais wa kwanza wa chama hicho kabla ya kufanikisha mapinduzi matukufu ya 12/01/1964.

Kumbuka, elimu ya Hayati huyu ni shule ya msingi lakini zaidi kilichomsukuma ni dhamira na fikra za ukombozi alizokuwa nazo. Zuhudi na umashuhuri wake utakumbukwa daima. Alipambana sana juu ya Uhuru wa Zanzibar. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Pia, tukimuangazia mkurugenzi wa kampuni ya Space X ambaye pia ndiye tajiri mkubwa duniani kwa sasa akiwa na ukwasi unaokadiriwa kuwa U$D 1950Billion, ambaye historia inamuelezea kwamba aliondoka kutoka nchini Afrika Kusini na kuelekea masomoni huko Marekani ambapo alitakuwa kwenda kuchukua masomo ya udaktari wa falsafa (Ph.D). Lakini siku mbili tu baada ya kuwasili nchini Marekani, aliona hali ni ngumu na akaamua kuondoka na kuacha masomo jumla. Inasemekana kwamba baada ya kuondoka masomoni tu, alitaamua kwenda kuanzisha makampuni ya kibiashara katika mtandao na hatimaye kuibuka kuja kuwa na bilionea mkubwa duniani.

Unahitaji maarifa kidogo tu ili kujiongezea uwezo wako wa kufikiri; au unahitaji ujinga kidogo tu ili uendelee kuishi gizani na ndani ya giza nene.

Mafanikio yapo kutokana na kile unachokiamini. Acha kukonyeza gizani kwa kuamua sasa kusimamia kile unachokiamini.  Konyezo la gizani huwa halimpati mlengwa, mathalani busu hewani!

Hutakiwi kusubiri mtu aje akuambie kwamba unatakuwa kuwa sehemu fulani zaidi, bali ni kuamka sasa na kuanza kupambania kile tunachokiamini.

Kila mtu ana lengo lakini lengo hilo hufubazwa na roho au tabia ya kughairisha mambo. Unahairisha kushughulikia changamoto zako mwenyewe, kupambania malengo yako mwenyewe.

Usipotumia ufahamau wako kufanikiwa kuwa wengine watautumia ufahamu wako kwa manufaa yao. Zinduka!

Unaweza ukaona karibu kila mlango unaojaribu kuugonga unaona haufunguki, jenga wa kwako. "If opportunities don't knock, build your own opportunity.

Weka lengo, tengeneza njia za kukufikisha kwenye lengo lako. Usikubali kukatishwa tamaa na elimu yako ndogo, ulemavu ulionao wala udhaifu unaoutazama. Kama ukitazama sana madhaifu yako utaishia kuwaonea donge wengine, hautafanikiwa. Anza kutazama zaidi fursa kuliko udhaifu wako. Udhaifu wako wa kimaumbile hauna uhusiano kabisa na mafanikio yako. Mwandishi wa kitabu cha "Don't Blame God" , Kenneth Hagin ambaye pia alikuwa mlemavu wa miguu, anakwambia kwamba hata ukiwa kilema wa miguu, bado unaweza kufanikiwa sana na kutembea mataifa mbalimbali ulimwenguni.

Ulemavu pekee wa kuuogopa ni ule wa akili tu, ogopa sana kulemaa akili. Akili ikilemaa, mwili ndiyo utakaosikilizia maumivu. Acha sasa, kataa kilema cha akili.

Ulemavu mwingine wote hauna nafasi kwenye mafanikio yako isipokuwa ule wa akili tu.

+255764987588

@Chief_Editor

#Msomi_Huru.


Comments

  1. Ni maarifa makubwa Sana na muhimu mno hususan kwa wasomi wengi wa Tanzania
    Wamebaki wakiamini kuwa ukiwa mwenye level kubwa ya kitaaluma ndio utakuwa umefanikiwa Katika maisha yako ya kila siku kumbe hata wale walioishia darasa la Saba waliweza kubadili Fikra zao kwa maarifa madogo na mwisho wa siku wakafanya Mambo makubwa mno Mimi binafsi nikushukuru ndugu Chief editor kwa makala hii nzuri kabisa

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

KWA NINI WATU WENGI HAWANA UTAMADUNI WA KUJISOMEA VITABU?

Mbwa Bado Hajafa! (Usikubali Kukata Tamaa)

KAULI KUMI ZA HAYATI MWL. JULIUS K. NYERERE KUHUSU ELIMU NDANI NA NJE YA NCHI