KINACHOKUFANYA USHINDWE KUFANIKIWA
Na; Mashaka Siwingwa
+255764987588
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Kinywa chako kinakuponza...
Hili nalo linakukwamisha usifanikiwe mpendwa!
Kila rafiki yako anapokosea lazima umseme kwa rafiki zako!
Kila anaponunua kitu kipya lazima umtangaze kwamba anajisikia! anajidai!
Kila mwenzako anapoteleza wewe ndiyo wa kwanza kutamba na kumwambia kwamba bila wewe asingeweza kuvuka!
Kila mwenzako anapopitia magumu na kukuomba msaada una mtangaza kwamba bila wewe asingepona! Mara oh asingefanikiwa!
Kwani wewe ni yupi?
Eti, wewe ni yupi?
Hiki ndicho kinachokuponza bro!
Yaani unatumia muda mwingi kuwabeza wenzako, kuwakatisha wenzako, kuwakera wenzako, kuwasema wenzako utafikiri huu ulimwengu umeumbiwa uishi milele... Hata maandiko matakatifu yanasema binadamu ni mavumbi na mavumbini atarudi! Unataka kuishi milele kisha utambe vizuri kwa idadi lukuki ya watu uliowasaidia?
Hata mitume na manabii wa zamani walitambua umuhimu wa kusaidiana katika maisha ndiyo maana Musa baada ya kugundua hivyo alianza kumuandaa Yoshua mapema!
Kwa hakika, haya maisha huwezi kusimama peke yako!
Ukitaka kuwa mkamilifu jenga dunia yako! Binadamu hukosea kisha hupata fursa ya kusahihisha makosa hayo. No body is perfect 100%!
Kwa namna yoyote ile, kwa gharama zozote zile, kwa hali yoyote Ile, amini usiamini, utake usitake, maisha hayawezi kwenda mpaka pale tutakapoziondoa fikra mufilisi na kuruhusu fikra pevu za kuwashirikisha na kushirikiana na wenzetu.
Huwezi kumlazimisha mwenzako awe mkamilifu wakati unafahamu fika kwamba binadamu tumeumbwa katika hali ya kujifunza! Hakuna mkamilifu.
Kwanini usianze wewe kukamilika?
Tatizo macho yako unayatumia kuwatazama wengine huku aibu ikikuangaza kujitazama wewe mwenyewe! Masikio yako yamekaa samawati kuyapokea ya wengine, umbea tu lakini siyo kusikia sauti itokayo ndani yako mwenyewe na kukuelekeza njia njema!
Huwezi kuwa mtu wa kuwachukia na kuwasema wengine wanapokosea halafu wewe ukikosea unakimbilia kuomba msamaha! Kama kukosea ni bahati mbaya basi umuwekee kinyongo mwenzako anapokukosea! Acha kabisa kauli za "Nimekusamehe ila sitakusahau". Sasa hapo kuna haja gani ya kumsamehe mtu? Samehe na sahau!
Badilika!
Mwenzako anapofanya vizuri jitahidi umpongeze, kama huwezi kumpongeza kaa kimya!
Mwenzako anapokosea jitahidi umsahihishe, kama huwezi kumsahihisha acha!
Jifunze utofauti uliopo kati ya kumkosoa mtu na kumsahihisha! Rafiki yako anapokosea unamsahihisha siyo unamkosoa!
Yeye siyo Mungu wa kuwa mkamilifu!
Wewe pia siyo masihi wa kujisifia kwa kuwasaidia watu wengine...
Kumbuka hata maandiko matakatifu yanasema unavyobariki ndivyo unavyobarikiwa!
Kumsema rafiki yako vibaya, kumsengenya, kumteta, kujiona bila wewe asingelifika hapo alipo siyo jambo jema hata kidogo! Kinywa chako ndiyo mchawi wa mafanikio yako... Sema ni vile tu umepigwa upofu hauwezi kuona wala kusikia.
Hayafai mtaani alisema Shaaban Robert katika diwani yake ya 'Mapenzi Bora'. Maisha lazima yaendelee hata usipokuwepo wewe! Jichunge, chunga kauli zako, chunga matendo yako!
Ewe kapuku uliyeshindwa kumtambua mchawi wako mwenyewe, mbona unataka kumnyooshea mwenzako kidole kimoja wakati vidole vinne vinakutazama wewe?
Fungua milango ya mafanikio yako kwa kubariki mafanikio ya wengine...
Jifunze namna walivyofanya mpaka wakafanikiwa maana mdomo wako utakuponza kwa maneno yako machafu... kumbuka maneno yana uwezo wa kuumba!
Siyo mwanamke mpumbavu tu anayebomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe hata rafiki mnafiki unazuia milango ya mafanikio yako mwenyewe!
Badilika!
Mashaka Siwingwa
+255764987588
Asnt kwa ujumbe mzuri
ReplyDeleteAsante kwa ujumbe mzur kwangu mie npata. Kitu kzr kitakachonisaidia maisha
ReplyDeleteUjumbe mzur sana Asante na Hongera
ReplyDeleteAhsante sana kwa ujumbe mzuli .
ReplyDeleteVery nice
ReplyDeleteUjumbe wenye afya umetufukia
ReplyDelete