Posts

HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUJIEPUSHA NA MAMBO YASIYOFAA

Kwenye maisha tunaishi na watu tofauti tofauti na wenye mitazamo tofauti tofauti. Watu hao huweza kuwa na mitazamo mizuri ama mibaya juu ya mambo fulani. Mathalani, hata wewe kuna baadhi ya mambo ukiyaona unaweza kuyapambanua kama ni mazuri au mabaya. Wakati mwingine hutakiwi hata kusubiri kuambiwa kama jambo hilo ni jema ama baya. Ni mara nyingi sana (kama siyo zote) kwa marafiki hupeana au kupashana habari au taarifa fulani. Taarifa au habari hizo huhusu mambo yanayozizunguka jamii hizo. Wakati mwingine marafiki huweza kusambaza habari hizo na kutuletea bila kuzipima kwa kina na kuweza kuzichuja ili kujua kama zinafaa au la! Na wakati mwingine habari hizo huwa hazifai kabisa kusambazwa! Kosa letu kubwa ni pale ambapo tunaamua kusambaza taarifa au habari ambazo tumezipokea tu kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki zetu bila kuweza kuzipima wala kuzichuja ili kuweza kujua uhalali wa habari hizo. Ikiwa tumepokea taarifa au habari zisizoaminika kutoka kwa marafiki zetu moja kwa moja tunaten...

SIFA KUU YA MTU MWONGO

Ukiwa mtu mwongo ni raha sana kwa sababu ukidanganya mara ya kwanza utatamani udanganye tena na tena. Uongo ni mtamu kuliko ukweli na ni rahisi kuusema kwa sababu unavutia na kufariji kwa muda mfupi. Muhimu tu ni kwamba ukiwa mwongo unatakiwa baada ya kudanganya mara ya kwanza, ya pili na ya tatu uwe na kumbukumbu, ukumbuke mara zote ulizodanganya tena kwa mpangilio ule ule. Zaidi, uwe na uwezo wa kuwakumbuka uliowadanganya; hapo ndipo unapokuja kukamatwa kwa sababu uongo hauna sifa ya kudumu.  Watu hujisahau mara tu baada ya kudanganya na huwa hawana uwezo wa kukumbuka tena. Ndiyo maana hata kwenye sheria (mahakamani) watu hukamatwa na hatia mara baada ya kuchanganya maelezo ya awali na yale yaliyofuatia. Unakuta mtu baada ya kueleza sentensi A anashindwa kuiunganisha na sentensi B na C kwa sababu sentensi A haikuwa na ukweli. Hivyo, anakuwa na uwezekano mkubwa wa kuchanganya mambo na kukutwa na hatia. Ndugu yangu, ukweli unahitaji vithibitisho vingi na vielelezo vingi ili kuweza ...

HIVI NDIVYO TUNAVYOWEZA KUSAPOTI WAHITIMU WAPYA KUANZISHA BIASHARA

Na:- Mashaka Siwingwa +255764987588 ____________________________________________________________________________________ Mnamo Juni 2021, niliweza kupokea kadi za aina tatu tofauti tofauti. Ninaweza kusema kwamba ulikuwa ni mwezi wa neema sana kwangu kiasi kwamba nilithaminiwa mpaka kufikia hatua ya kupewa kadi. Kadi ya kwanza ilikuwa imenakshiwa safi kabisa kwa rangi ya mzambarau. Ilikuwa ni kadi nzuri na yenye kuvuti. Ilikuwa ni kadi iliyoambatanishwa na jina langu kabisa tena kwa herufi kubwa. Baada ya kuifungua na kuisoma ilikuwa ikinitaka kuchangia harusi ya rafiki yangu ambaye alitarajia kufunga pingu za maisha Oktoba, 2021. Nilimshukuru sana Mungu kwa kitendo cha mimi kuonekana wa maana mpaka kufikia hatua ya kupewa kadi ya kuchangia harusi. Hiyo niliiweka chini. Baada ya kuiweka chini niliichukua kadi ya pili. Hii ilionekana kuwa ya hadhi ya chini kidogo na haikupambwa sana kama ile ya awali. Niliipokea kutoka kwa rafiki yangu wa karibu. Nilivyoifungua na kuisoma niligundua kwa...

TOFAUTI KUBWA ILIYOPO KATI YA UONGOZI NA CHEO

Mara nyingi watu huchanganya kati ya hizi dhana mbili. Watu wengi hudhani kwamba ziko sawa na wachache hudhani kwamba zinatofautiana. Ndiyo! Inawezekana zipo sawa au zinatofautiana kulingana na namna unavyozitafsiri dhana hizi.  Siku ya leo ninaomba niwasaidie wale wanaojua dhana hizi zinaendana 100% na hawawezi kabisa kutofautisha kati ya dhana hizi. Uongozi ni madaraka anayopewa mtu ya kusimamia au kuongoza. Au ni majukumu ambayo mtu hukabidhiwa ili ayatekeleze. Kwa upande mwingine tuna istilahi 'Cheo.' Istilahi hii ina maana nyingi kwa mujibu wa waandishi mbalimbali na kamusi mbalimbali za lugha ya kiswahili. Kwa mujibu wa kamusi moja inasema 'Cheo' ni nafasi ya hadhi ambayo mtu anapewa kazini. Lakini pia kuna maana isemayo 'Cheo' ni ubao utumikao kusukia ukili. Zaidi ni kwamba kuna tafsiri nyingi sana na nyingine ni tofauti sana na lengo letu. Sasa lengo letu ni kutofautisha dhana ya cheo kama hadhi ya heshima anayopewa mtu na uongozi kama dhamana ya majukum...

UKITAKA WATU WAKUHESHIMU FANYA HIVI

Kila mtu anastahili kupewa heshima na kuthaminiwa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba heshima na thamani ni kitu ambacho kila mtu anastahili. Haijalishi elimu zetu, tamaduni zetu, makabila yetu, dini zetu wala maeneo tunayotokea. Kutokuheshimiana ni moja ya kitu ambacho kimekuwa kikisababisha migogoro kwa watu mbalimbali. Mtu mmoja anaposhindwa kumheshimu mwenzake hupelekea migogoro na hata kuvunja ukaribu wao. Marafiki wawili wanaposhindwa kuheshimiana huwa hawana haja tena ya kuona kama urafiki wao una manufaa yoyote yale bali huamua kuvunja urafiki wao. Wapenzi wengi pia wanaposhindwa kuheshimiana hupelekea mogogoro kwenye mapenzi yao na hata kuvunja mahusiano. Mathalani, wanandoa wanaposhindwa kuheshimiana na kuthaminiana hupelekea  migogoro ndani ya nyumba na hatimaye kuamua kuvunja mahusiano au ndoa yao. Kwa kawaida, suala la kutoheshimiana ni suala la mtu mmoja mmoja kwani ni matokeo ya ubinafsi baina yetu. Kwa mujibu wa Dkt. Issaya Lupogo & Aziza Lupogo (2019) katika kita...

SAA ZA KIBONGO DHIDI YA SAA ZA KIZUNGU: WABONGO TUNAZINGUA SANA

Na: Mashaka Siwingwa __________________________________________ "Do you love life? Then do not squander time; for it is the stuff that life is made of." Ilikuwa ni kauli ya Benjamin Franklin kama alivyonukuliwa na Brian Tracy katika kitabu chake cha Time Power. Siku hizi wabongo tumetumbukia katika balaa; naam balaa zito kwelikweli. Balaa la kushindwa kuwa na nidhamu; nidhamu katika matumizi ya muda. Siku hizi kuna muda wa kibongo na muda wa kizungu. Mtu akikwambia tukutane saa saba kamili saa za kibongo basi ujue hiyo ni saa tisa kama siyo saa kumi na nusu. Mtu akikwambia tukutane saa nane kamili saa za kizungu basi ujue hiyo ni saa nane kamili kama ilivyotajwa. Hizi kauli za "saa za kibongo"  na "saa za kizungu"  tumezitengeneza wenyewe aidha kwa kujua au kutokujua. Tumekuwa tukiwaabudu wazungu bila kujua kwa sababu tunakubali kila kilicho cha kwao.   Saa za kibongo ni ishara ya dharau na kukosa uaminifu wakati saa za kizungu ni uaminifu na "commitm...

"MUUZA KIFO AFARIKI DUNIA"

Kaka wa mtengeneza silaha maarufu duniani, Alfred Nobel alifariki dunia na waandishi wa habari wakaibuka na kuandika, "Muuza Kifo Afariki Dunia"  Awali, waandishi wa habari waliamini kwamba aliyefariki ni Alfred Nobel ambaye alikuwa ni mtengeneza mabomu na silaha za moto kwa kutumia madini ya dainamaiti. Alfred Nobel alikuwa mtengenezaji mabomu wa dainamaiti na alifanya kazi hiyo kama sehemu yake ya kujiingizia kipato. Ulimwengu ulimchukia kwa sababu aliuza kifo na kwa bahati mbaya hakufanikiwa kung'amua kitu cha namna hii.  Alfred Nobel aliishi maisha ya furaha sana kwa kuwa na kipato kizuri kupitia kuuza silaha hizo hatari. Kwa bahati mbaya ni kwamba hakufanikiwa kujua namna ambavyo alikuwa anachukiwa na jamii yake kwa kazi hiyo haramu. Baada ya miaka kadhaa kupita, kaka yake alifariki na waandishi wa habari baada ya kupata habari hizo wakajua aliyefariki ni Alfred aliyekuwa akitegemea kazi ya kutengeneza mabomu na silaha kama sehemu yake ya kujiingizia kipato. Waandish...