KUJUA SIYO KUTENDA, TUJITATHIMINI
Na; Mashaka J. Siwingwa +255764987588 ----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------- Ukienda kanisa lolote lile lazima utakutana na watu wa aina tatu. Wale walio moto kwenye masuala ya kikanisa, wale ambao ni vuguvugu na wale ambao ni baridi kabisa. Watu ambao wako moto kwenye masuala ya kikanisa, wao hushiriki katika kila shughuli ya pamoja, huweza kuhamasisha na kuwatia moyo wengine ili waweze kushiriki pia, hawa hawakati tamaa na ni waaminifu sana kwenye masuala ya kiimani japokuwa kuna changamoto za kiubinadamu pia. Mara nyingi hawa huwa ni viongozi. Watu ambao ni vuguvugu, wao husubiria hamasa kwenye kila jambo ili waweze kushiriki katika shughuli fulani. Wao husubiri watengenezewe mazingira ya urahisi au ugumu wa jambo fulani ndipo waamue kama waliunge mkono au walipige kipepsi. Hawa watu mara nyingi wanahoji sana. Kwa mfano, kiongozi yeyote yule wa kanisa anapotangaza maombi ya mfungo wa wiki m...