MIPANGO NI MATANGO; UKIILAZA ITAOZA
Habari yako mpenzi mfuatiliaji wa makala kutoka katika blogu hii. Napenda nikukaribishe tena kusoma makala hii ya leo. Makala ya leo ni fupi sana lakini iliyobeba ujumbe.
Naam, pengine umewahi kuweka mipango yako ambayo umeona ni vema kama ukiitimiza ndani ya muda fulani. Labda ni ndani ya mwezi, miezi kadhaa, mwaka au baada ya miaka kadhaa.
Napenda kukuthibitishia tu kwamba muda unakwenda na wala haurudi. Siku nazo zinazidi kusonga mbele kiasi kwamba usipokuwa makini utajikuta umefika mwisho wa malengo yako na hujafanya chochote.
Ninakushauri tu upange malengo ya muda mfupi kabla ya kufikia malengo ya muda mrefu. Unaweza kuanza kwanza kupanga malengo yako kwa siku, mwezi na hata mwaka.
Njia hii itakusaidia kurahisisha mipango yako ili usije kufikia siku ya mwisho hujafanya chochote. Lazima uwe na mbinu mbadala za kufikia malengo yako.
Ahsante sana.
Imeandikwa na;
Mashaka J. Siwingwa.
Very nice Good job
ReplyDelete