Posts

Showing posts from February, 2021

USISAHAU KUFANYA HIVI KILA BAADA YA HATUA MOJA.

Na; Mashaka Siwingwa +255764987588 ----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------- Kufanikiwa siyo mpaka ufikishe 100% ya malengo yako. Unaweza kufikia 5% ya matarajio na bado ikawa ni sehemu ya mafanikio kulingana na malengo yako. Sasa baada ya kupiga kila hatua, jitahidi kuota moto na waliokusaidia kukusanya kuni. Hakuna mtu anayefanikiwa kwa juhudi zake mwenyewe. Hii ni  kutokana na ukweli kwamba hakuna mtu anayeishi kwenye ulimwengu wake mwenyewe.  Katika safari ya mafanikio lazima kuna watu ulikutana nao wakakuonyesha njia, wakakupatia maji ya kunywa njiani, wakakupa chakula, wakakupokea mizigo na kukupa hifadhi ya kulala. Japo siyo wote maana lazima kuna wengine waliokutukana, kukudhihaki, kukucheka, kukudharau na  kukuhakikishia kwamba hutaweza kufanikiwa. Sasa leo mshukuru Mungu kwa sababu walikupandisha hasira. Wakati unamshukuru Mungu kwa ajili ya hili kundi la pili, likumbuke kundi la...

MFAHAMU SAMORA MOISES MACHEL; SHUJAA WA MSUMBIJI.

Na; Mashaka Siwingwa +255764987588 -----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------  IIikuwa mnamo 20 October,1986 siku ambayo haitasahaulika katika nyoyo za raia wengi wa Msumbiji na Afrika hasa katika nchi zilizokuwa mstari wa mbele katika ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika, Tanzania ikiwa mmojawapo. Ni siku ambayo Samora Moises Machel, Rais wa Kwanza wa Msumbiji na maofisa wengine 33 walikuwa angani wakitokea Zambia kurudi Msumbiji wakati ndege yao ya Kisovieti aina ya Tupolev ilipoanguka nchini Afrika Kusini. Utawala wa Afrika Kusini wa wakati huo wa Wazungu wachache na washirika wao wa Magharibi ulidai kuwa ajali hiyo ilitokana na uzembe wa wafanyakazi wa ndege hiyo. Lakini Msumbiji, Urusi na mataifa mengine mengi ya Afrika, yaliamini kabisa ilikuwa ya kupangwa na uchunguzi ulibainisha hilo. Msumbiji pia ilikumbushia vitisho vya utawala huo kandamizi dhidi ya maisha ya Machel, vilivyotolewa na aliy...

MSINGI MZURI WA HATMA YAKO NI WEWE MWENYEWE.

__________________________________________ Ukisoma maneno yaliyoandikwa hapo juu unaweza usiyaelewe kwa haraka lakini hayajakosewa kabisa. Mheshimiwaa Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete aliwahi kusema; ukitaka kula ukubali kuliwa... Akiwa na maana ya kwamba ili upate faida lazima ulipe gharama fulani hivi na kauli hii ina ukweli ndani yake kabisa kwani huwezi kuvuna mazao kama haukufukia mbegu ardhini. Katika jamii kuna watu wa namna mbalimbali sana, mathalani watu tunatofautiana kirangi, kimwili, kimaumbile, kijinsia na hata kiuchumi.  Leo ninaomba kuwazungumzia watu wa namna mbili tu ambao wamejaaliwa vipawa fulani lakini wanapishana namna ya kuvitumia vipawa hivyo; 1. Watu wanaotaka wapewe vitu ili waonyeshe walivyonavyo (vipawa vyao); Hawa ni watu ambao hukaa na vipawa vyao au talanta walizonazo. Huwa wanasubiri mpaka mtu aseme anatafuta watu wenye uwezo wa kuimba ndipo wajitokeze. Wakikosa mtu wa kusema hivyo huua talanta zao. Watu wa aina hii ni wepesi sana kukata tamaa pal...

KATIKA SIASA: HAWA HAPA MAWAZIRI WAKUU WA TANZANIA TANGU UHURU HADI SASA

_______________________________________ Habari yako mpenzi mfuatiliaji wa makala mbalimbali kutoka katika jamvi hili? Natumai u mzima na bukher wa afya...  Leo nimeona ni vyema nikupitishe kidogo katika historia kwa kukufahamisha mawaziri wakuu wa taifa hili tangu Uhuru mpaka sasa. Nimeamua kufanya hivi kama ishara ya kuonyesha uzalendo kwa taifa letu maana ni muhimu kuifahamu historia ya taifa letu. Fuatana nani sasa; 1. MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE Huyu ndiye Waziri Mkuu wa kwanza kabisa wa Tanzania (Tanganyika). Alitawala tangu Septemba 2, 1960 mpaka Mei 1, 1961 kabla ya kuchaguliwa mara ya pili Mei 1, 1961 mpaka Januari 22, 1962, Tanganyika ilipokuwa jamhuri.  2. RASHID MFAUME KAWAWA. Huyu ndiye Waziri Mkuu wa pili wa Tanganyika ( baadaye Tanzania). Alitawala tangu Januari 22, 1962 mpaka Desemba 9, 1962. Aliteuliwa tena kukalia kiti hicho mnamo Februari 17, 1972 mpaka Februari 12, 1977. 3. EDWARD MORINGE SOKOINE. Huyu ndiye aliyekuwa Waziri Mkuu wa tatu wa Tanzania. Al...

HAUNA CHA KUPOTEZA UNAPOWEKEZA KATIKA UTU

Ndiyo, utu ni dhana mtambuka sana na ambayo kila mtu anao uwezo wa kuielezea kutokana na namna anavyoielewa yeye. Mara nyingi tafasiri hizo zinaweza kuhusishwa na maoni ya mtu binafsi au la juu ya namna anavyoichukulia dhana ya neno 'utu'. Kwangu mimi, utu ni zawadi bora kabisa ambayo mtu hupewa na mwenyezi Mungu. Ni zawadi bora kuwahi kutokea ulimwenguni. Hii ndiyo zawadi pekee inayoweza kutumika kuua, kuvunja na kuharibu matabaka yaliyopo kwenye jamii; tajiri dhidi ya masikini, kilema dhidi ya asiye kilema, msomi dhidi ya asiyesoma, mkulima dhidi ya daktari n. k.  Ni dhana pekee ambayo inapotamkwa hujenga fikra fulani za msawazo kuashiria kwamba binadamu wote ni sawa mbele za Mungu ukitupilia mbali nafasi zetu za kijamii tulizonazo, nafasi za kiuchumi na hata nafasi za kisiasa. Tunu ya 'utu' ni tunu adimu na adhimu sana kuwahi kutokea ulimwenguni na ni tunu ambayo imewekwa kwa mtu mmoja mmoja; siyo kwa kikundi. U-tunu wa neno 'utu' unaanzia kwenye sifa au tabi...

HEBU NIAMBIE HAPA; JE, KOSA NI LA NANI?

Jumanne, 02.02.2021 U hali gani mpenzi mfuatiliaji wa makala mujaarabu kutoka MSOMI HURU BLOG? Leo nimeamua kukuandalia hii simulizi fupi sana lakini yenye jambo la kujifunza.  Tafadhali ninaomba baada ya kusoma tushirikishane maarifa; niambie, unadhani tatizo ni la nani? Karibu; __________________________________________ Siku moja bwana Kanjunju alikwenda kituo cha afya kucheki afya yake. Alipofika alibahatika kumuona daktari moja kwa moja. Baada ya kuingia ndani akawa amechukuliwa vipimo na kuruhusiwa kutoka nje ili asubirie majibu ya vipimo vyake. Aliendelea kusubiri majibu ya vipimo vyake kwa takribani dakika kadhaa. Hatimaye aliingiwa na uchovu, akachoka kusubiri. Wakati amekaa kwenye korido akaamua kutoa  simu yake janja ili aangalie nini kimejiri mtandaoni. Kama unavyojua dunia inakuwa Kijiji ukiwa na simu janja ya kiganjani. Mtandao wa kwanza kuufungua ulikuwa ni WatsApp. Ile anafungua tu akakutana na group jipya; "VVU IKONJE DISPENSARY" kabla hajafanya chochote akaan...