HEBU NIAMBIE HAPA; JE, KOSA NI LA NANI?
Jumanne, 02.02.2021
U hali gani mpenzi mfuatiliaji wa makala mujaarabu kutoka MSOMI HURU BLOG?
Leo nimeamua kukuandalia hii simulizi fupi sana lakini yenye jambo la kujifunza.
Tafadhali ninaomba baada ya kusoma tushirikishane maarifa; niambie, unadhani tatizo ni la nani?
Karibu;
__________________________________________
Siku moja bwana Kanjunju alikwenda kituo cha afya kucheki afya yake. Alipofika alibahatika kumuona daktari moja kwa moja. Baada ya kuingia ndani akawa amechukuliwa vipimo na kuruhusiwa kutoka nje ili asubirie majibu ya vipimo vyake.
Aliendelea kusubiri majibu ya vipimo vyake kwa takribani dakika kadhaa. Hatimaye aliingiwa na uchovu, akachoka kusubiri.
Wakati amekaa kwenye korido akaamua kutoa simu yake janja ili aangalie nini kimejiri mtandaoni. Kama unavyojua dunia inakuwa Kijiji ukiwa na simu janja ya kiganjani.
Mtandao wa kwanza kuufungua ulikuwa ni WatsApp. Ile anafungua tu akakutana na group jipya; "VVU IKONJE DISPENSARY" kabla hajafanya chochote akaanguka chini puuuh!!
Watu waliokuwa pale wakafanya utaratibu wa kumuita daktari, kwa sababu daktari alikuwa na shughuli nyingine huko chumbani kwake hivyo alichelewa kidogo.
Presha ilimpanda bwana Kanjunju kisha akafariki dunia. Baada ya daktari kufika aliufanyia uchunguzi mwili wa marehemu. Akagundua kwamba marehemu amefariki kwa presha!
Je, nani amemuua bwana Kanjunju?
Pia, kuna jambo gani la kujifunza kupitia kisa hiki?
KARIBU UTOE MAONI
#powered by
MSOMI HURU FOUNDATION
Kabla cjakoment nani aliyemuadd kwenye hilo group la whatsAap
ReplyDeleteGenerally kosa ni la kanjunju kwani huwezi unaona group na kumaanisha huenda ujumbe ulokuwemo haukumuhusu yeye kanjunju
Hatuwezi kujua inawezekana daktari ndiye aliyemu-add maana tayari alikuwa na majibu ya vipimo vyake.
ReplyDelete