KATIKA SIASA: HAWA HAPA MAWAZIRI WAKUU WA TANZANIA TANGU UHURU HADI SASA
_______________________________________
Habari yako mpenzi mfuatiliaji wa makala mbalimbali kutoka katika jamvi hili?
Natumai u mzima na bukher wa afya...
Leo nimeona ni vyema nikupitishe kidogo katika historia kwa kukufahamisha mawaziri wakuu wa taifa hili tangu Uhuru mpaka sasa. Nimeamua kufanya hivi kama ishara ya kuonyesha uzalendo kwa taifa letu maana ni muhimu kuifahamu historia ya taifa letu.
Fuatana nani sasa;
1. MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE
Huyu ndiye Waziri Mkuu wa kwanza kabisa wa Tanzania (Tanganyika).
Alitawala tangu Septemba 2, 1960 mpaka Mei 1, 1961 kabla ya kuchaguliwa mara ya pili Mei 1, 1961 mpaka Januari 22, 1962, Tanganyika ilipokuwa jamhuri.
2. RASHID MFAUME KAWAWA.
Huyu ndiye Waziri Mkuu wa pili wa Tanganyika ( baadaye Tanzania).
Alitawala tangu Januari 22, 1962 mpaka Desemba 9, 1962.
Aliteuliwa tena kukalia kiti hicho mnamo Februari 17, 1972 mpaka Februari 12, 1977.
3. EDWARD MORINGE SOKOINE.
Huyu ndiye aliyekuwa Waziri Mkuu wa tatu wa Tanzania.
Alihudumu katika kiti hicho kwa awamu ya kwanza mnamo Februari 13, 1977 mpaka Novemba 7, 1990.
Aliteuliwa kwa mara nyingine tena kushika wadhfa huo mnamo Februari 24, 1983 mpaka Aprili 12, 1984.
4. CLEOPA DAVID MSUYA.
Ni Waziri Mkuu wa nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alihudumu katika kiti hicho kwa mara ya kwanza mnamo Novemba 7, 1980 mpaka Februari 24, 1983.
Aliteuliwa tena kukalia kiti hicho kwa mara ya pili mnamo Desemba 7, 1994 mpaka Novemba 28, 1995.
5. SALIM AHMED SALIM.
Huyu ndiye Waziri Mkuu wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alihudumu katika kiti hicho tangu 1984 mpaka 1985.
6. JOSEPH SINDE WARIOBA.
Alikuwa Waziri Mkuu wa sita wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alidumu katika wadhfa huo kwa miaka mitano.
Aliteuliwa mnamo mwaka 1985 na kuachia kiti hicho mnamo mwaka 1990.
7. JOHN MARECELA.
Waziri Mkuu wa saba wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alihudumu katika nafasi hiyo tangu mnamo mwaka 1990 mpaka mwaka 1994.
8. FREDERICK SUMAYE.
Huyu ndiye Waziri Mkuu wa nane wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ndiye Waziri Mkuu wa kwanza kukaa katika kiti hicho kwa muda mrefu.
Alitumikia umma katika wadhfa huo kwa miaka kumi.
Alihudumu tangu mnamo mwaka 1995 mpaka mwaka 2005.
9. EDWARD NGOYAI LOWASSA.
Alikuwa Waziri Mkuu wa tisa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alihudumu katika nafasi hiyo kwa miaka mitatu tu. Alilazimika kuachia nafasi hiyo kutokana na tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
Alihudumu tangu mwaka 2005 na kujiuzuru mnamo mwaka 2008.
10. MIZENGO KAYANZA PINDA.
Huyu ndiye Waziri Mkuu aliyewahi kuwa na kauli za kibabe nchini.
Alikuwa ni Waziri Mkuu wa kumi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alihudumu katika nafasi hiyo tangu mwaka 2008 (baada ya Lowassa kujiuzuru) mpaka mwaka 2015.
11. KASSIM MAJALIWA.
Waziri Mkuu wa kumi na moja wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aliingia madarakani katika nafasi hiyo tangu mwaka 2015 mpaka sasa.
Anasifika kwa kuwa na maamuzi magumu pamoja na utumishi uliotukuka.
Hao ndiyo mawaziri wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu wa kwanza mpaka wa sasa.
Mungu ibariki Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mungu wape pumziko la milele waheshimiwa mawaziri wakuu wote waliotangulia mbele za haki.
Amina...Endelea kufuatilia makala kutoka msomihurublog.blogspot.com ambazo zimekuwa zikitumwa kila baada ya siku moja.
Ahsante!
#Chief_Editor
@Msomi_Huru.
Comments
Post a Comment