USISAHAU KUFANYA HIVI KILA BAADA YA HATUA MOJA.

Na; Mashaka Siwingwa

+255764987588

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Kufanikiwa siyo mpaka ufikishe 100% ya malengo yako. Unaweza kufikia 5% ya matarajio na bado ikawa ni sehemu ya mafanikio kulingana na malengo yako.

Sasa baada ya kupiga kila hatua, jitahidi kuota moto na waliokusaidia kukusanya kuni.

Hakuna mtu anayefanikiwa kwa juhudi zake mwenyewe. Hii ni  kutokana na ukweli kwamba hakuna mtu anayeishi kwenye ulimwengu wake mwenyewe. 

Katika safari ya mafanikio lazima kuna watu ulikutana nao wakakuonyesha njia, wakakupatia maji ya kunywa njiani, wakakupa chakula, wakakupokea mizigo na kukupa hifadhi ya kulala.

Japo siyo wote maana lazima kuna wengine waliokutukana, kukudhihaki, kukucheka, kukudharau na  kukuhakikishia kwamba hutaweza kufanikiwa. Sasa leo mshukuru Mungu kwa sababu walikupandisha hasira.

Wakati unamshukuru Mungu kwa ajili ya hili kundi la pili, likumbuke kundi la kwanza kwa kusimama na wewe katika wakati mgumu maana walikutia moyo, walikusaidia na walikufariji pale uliposhindwa. 

Wakumbuke kwa kuwashukuru hata siku moja kwa kuwa hawakukata tamaa kukutia moyo katika safari yako.

Kwa kufanya hivyo, utakuwa umetuma mwaliko wa baraka kutoka kwao na kwa mwenyezi Mungu pia.

Kumbuka kushukuru waliosimama na wewe wakati wa dhiki. 

Mashaka Siwingwa

Mzumbe University

+255764987588.

Comments

Popular posts from this blog

KWA NINI WATU WENGI HAWANA UTAMADUNI WA KUJISOMEA VITABU?

Mbwa Bado Hajafa! (Usikubali Kukata Tamaa)

KAULI KUMI ZA HAYATI MWL. JULIUS K. NYERERE KUHUSU ELIMU NDANI NA NJE YA NCHI