KILA MTU NI GENIUS; JE, WEWE NI GENIUS WA KITU GANI?
"Everyone is a genius but if you judge a fish by it's ability to climb a tree, it will live its whole life believing that it is stupid". Hii ilikuwa ni kauli ya Albert Einstein akiwa na maana ya kwamba; " Kila mtu ni genius, lakini kama ukimhukumu samaki kwa kushindwa kupanda juu ya mti basi ataishi maisha yake yote akiamini kwamba hana akili". Mungu alipokuleta duniani, alihakikisha kwamba ameweza kuweka uwezo wa pekee sana ambao mara tu utakapougundua na kuanza kuufanyia kazi utakuletea matokeo makubwa sana. Watu wengi wanazaliwa na hadi wanaondoka duniani hawajajua uwezo wao huu wa kipekee uliojificha ndani yao na matokeo yake wanaishia kuwa watu wa kawaida sana. Ndiyo maana unawakuta watu wengi wanakata tamaa wakifeli masomo na mitihani mbalimbali. Mathalani hata jamii umekuwa ikiwazomea kwa kushindwa katika mitihani hiyo! Mbona hujiulizi kwanini watu wengi waliofanikiwa hawakuwa na uwezo mkubwa darasani? Moja ya hatari kubwa sana ya kutojua uwezo wako ni ku...