USIOGOPE, WEWE SI WA KWANZA KUWEKEWA VIKWAZO.

Tangu mnamo mwaka 1917 nchi ya Marekani imekuwa ikiliwekea vikwazo kadhaa vya kiuchumi taifa dogo la Cuba.

Baadhi ya mikataba mbalimbali ilisainiwa ili kumuondoa Cuba kwenye ramani ya ushindani kiuchumi lakini mpaka leo bado anadunda tu!


Kwa uchache tu, mikataba hiyo ni kama vile: 

-Trading with the Enemy Act of 1917.

-The Foreign Assistance Act of 1961.

-The Cuban Assets Control Regulations of 1963.

- The Torricelli Act of 1992.

-The Helms-Burton Act of 1996

- The Trade Sanction Reform and Export Enhancement Act of 2000.

- The U.S Commission for Assistance to a Free Cuba of 2004 and 2006.

Naomba kunukuu kidogo hapa;

" According to the U.S government... The embargo on Cuba is the most comprehensive set of American sanctions ever imposed upo  a country. (The Economic War Against Cuba_ A Historical and Legal Perspective on the U.S Blockade ,2013).


Hapo juu ni baadhi tu ya mikataba iliyosainiwa ili kumuwekea vikwazo Cuba lakini mpaka leo bado anatikisa tu mtaani. Historia inaonyesha kwamba tangu kupinduliwa kwa Fulgensio Batista na Fidel Castro, Cuba haijawahi kutikiswa mpaka leo. Mwanaume alitafutwa kwa kila mtega bila mafanikio (Castro). Walijaribu kumletea mwanamama ambaye hata hivyo aliishia kuolewa na kusitisha mpango wake wa kumuua Castro. Hatimaye mwamba alifariki uzee akiwa na umri wa miaka 90. 


Martin Luther King Jr anakwambia kama huwezi kutembea basi kimbia, kama huwezi kukimbia basi tambaa, kama huwezi kutambaa.... Lakini  kwa namna yoyote ile, uhakikishe unasonga mbele.


Wakikuletea dharau chukua, weka mfukoni, maisha yaendelee. Pambana bila aibu mpaka ifike wakati vikao vya familia visifanyike bila wewe kuwepo!


#Chief_Editor

MSOMI HURU

Comments

Popular posts from this blog

KWA NINI WATU WENGI HAWANA UTAMADUNI WA KUJISOMEA VITABU?

Mbwa Bado Hajafa! (Usikubali Kukata Tamaa)

KAULI KUMI ZA HAYATI MWL. JULIUS K. NYERERE KUHUSU ELIMU NDANI NA NJE YA NCHI