KUELEKEA 2021, JIWEKEE AHADI JUU YA HAYA MAMBO KUMI

Natambua kwamba tupo mwishoni mwa mwaka 2020 na tunakwenda kuupokea mwaka 2021 hivi punde. Inawezekana mwaka 2020 haukuwa wa furaha kwako, haukuwa wa mafanikio kwako, mambo mengi uliyopanga hayakufanikiwa. Naomba tunapokwenda kuingia mwaka mpya ukajiwekee ahadi zifuatazo wewe mwenyewe bila kusukumwa na mtu. Ni matumaini yangu, ahadi hizi zitafanyika msaada kwako:

1. Jiahidi wewe mwenyewe kuwa imara kiasi kwamba hakuna kitu kinachoweza kuutikisa ufahamu wako.

2. Jiahidi wewe mwenyewe kuwa mtu mwenye afya, amani, mafanikio na furaha kwa mtu yeyote utakayekutana naye maishani mwako.

3. Jiahidi wewe mwenyewe kuwafanya marafiki zako kwamba kuna kitu wanacho katika fahamu zao, hawako watupu.

4. Jiahidi wewe mwenyewe kufanya yaliyobora, kwa kufiri kwa namna iliyobora na kwa manufaa bora.

5. Jiahidi wewe mwenyewe kujifunza kupitia mafanikio ya wengine huku ukiamini kwamba na wewe upo njiani kufanikiwa.

6. Jiahidi kusahau makosa ya zamani huku ukitarajia kupata mafanikio makubwa sana mbeleni.

7. Jiahidi wewe mwenyewe kuvaa sura ya ucheshi na kutabasamu mbele ya kila mtu unayekutana naye.

8. Jiahidi wewe mwenyewe kutumia muda mwingi kuboresha mapungufu yako huku ukiamini kwamba huna muda wa kuwakosoa wengine.

9. Jiahidi wewe mwenyewe kuwa mkubwa kuliko uoga, mstaarabu kuliko hasira, imara kuliko mashaka na mwenye furaha kufagia chembechembe za chuki.

10. Jiahidi wewe mwenyewe kutoshindwa katika maisha yako. Hii itakusaidia kukuongezea nguvu za ushindani dhidi ya changamoto za maisha.


Comments

  1. Elimu kubwa xn hivyo tuite akili kubwa kuonesha njia ya kuelekea kwa bwana mafanikio

    ReplyDelete
  2. Mawazo kuntu hope yatatusaidia 2021

    ReplyDelete
  3. Ni mawazoo mazuri saaana tanajenga ujasuri ukiyatendea kazi

    ReplyDelete
  4. Mawazo mazuri sana na tutayafanyia kazi nwenyezi MUNGU akubariki sana kwa kuchukua muda wako kwa kutaandalia kitu kizuri kama hiki

    ReplyDelete
  5. Asante ndugu Mungu na akubariki na akuongezee pale ulipo punguza nimepata vitu vingi sana hapa vya kuinuka navyo katika uandishi wako hapa asnte sana

    ReplyDelete
  6. Makala safi nimejifunza mema mengi, Kongole kwako mwalimu Siwingwa

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

KWA NINI WATU WENGI HAWANA UTAMADUNI WA KUJISOMEA VITABU?

Mbwa Bado Hajafa! (Usikubali Kukata Tamaa)

KAULI KUMI ZA HAYATI MWL. JULIUS K. NYERERE KUHUSU ELIMU NDANI NA NJE YA NCHI