Posts

SABABU KUBWA (06) KWA NINI WAFANYABIASHARA 'WANAOJITAMBUA' WANATUMIA BUSINESS CARDS

Image
 Yes, unaweza kuonekana ni mtindo mgeni wa maisha lakini hii ni moja kati ya njia rahisi sana za kufanya marketing ya biashara au huduma yako. Matumizi ya business cards katika kutangaza biashara au huduma yako yana faida kadhaa kubwa sana.  Hapa chini ni faida chache tu! Mosi, business cards huonesha smartness kwenye ufanyaji wa biashara au utoaji wa huduma yako. Mtu yeyote yule anapokuomba mawasiliano yako ukampatia business cards; moja kwa moja anajua kwamba upo serious na unajua vyema unachokifanya. Pili, business cards hujenga uaminifu. Wateja wengi hukuamini wewe pamoja na huduma au biashara yako hasa mara baada ya kujiridhisha kwamba uko formal sana.  Tatu, huongeza ujasiri. Unapotumia business cards kuendesha huduma au biashara yako, hii inakuongezea ujasiri hata wewe mwenyewe hasa pale ambapo mtu anakuomba contacts unampatia business cards 😎 Nne, ni njia mojawapo ya kutangaza biashara au huduma unayofanya. Tuchukulie mfano umekutana na ndugu ambaye muda mrefu ha...

Je, Huyu ni Wewe?

Image
Je, unahitaji kudesign na kuprinti stickers? Je, unahitaji kudesign na kuprinti vitabu vya tickets? Je, unahitaji kudesign na kuprinti ID Cards? Je, unahitaji kuprinti t-shirts? Je, unahitaji kudesign na kuprinti vitabu vya risiti (receipt books)? Je, unahitaji kudesign na kuprinti flyers? Je, unahitaji kudesign na kuprinti business cards? Je, unahitaji kudesign na kuprinti vitabu vya malipo (payment vouchers)? Wala Usipate Shida... ... Msomi Huru Enterprises Co. LTD ndiyo jibu lako! Tunafanya designing za ubora wa hali ya juu pamoja na printing aina zote (zenye viwango vya TBS) Tunakukaribisha sana kufanya kazi na sisi na kwa hakika, HAUTAJUTA KUTUAMINI📌 Wasiliana nasi kwa simu namba: 0764 987 588 Barua pepe:  msomihurugroup@gmail.com Tupo Mzumbe - Morogoro Karibuni Sana!

HIZI HAPA SABABU 100+ KWA NINI UNATAKIWA UKUZE BRAND YAKO KWANZA NDIPOSA UONE MAFANIKIO YAKITIRIRIKA KAMA MAJI YA MTO YORDANI!

Image
  Watu wengi sana ambao ni wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali huwa wanajikuta wakiwa kwenye mkanganyiko mkubwa mkubwa sana wa kipi wanachotakiwa kufanya kati ya kukuza brand zao kwanza ama kuendelea kutoa huduma tu. Wengine hukaribia hata kiasi cha kukata tamaa hasa pale wanapokuwa hawaoni matokeo ya kile wanachokifanya. Ukweli ni kwamba, ni muhimu sana kukuza brand yako wakati unaendelea kutoa huduma ama kufanya biashara zako ili watu waweze kukuamini na kufanya kazi na wewe ama kununua kutoka kwako. Hii inasaidia kiasi kwamba unafika wakati ambapo wateja wakiwa na uhitaji mbalimbali lazima waje kununua kutoka kwako kwa sababu ya brand yako. Wakati mwingine kinachokusaidia kuuza au kupata wadau siyo aina ya bidhaa zako unazotoa, bali ni kwa sababu ya brand au jina lako linavyofahamika. Habari njema ni kwamba, hata wewe unayonafasi kubwa sana ya kupambania brand yako wakati unaendelea kufanya biashara yako. Brand itakutangaza na kukufanya uaminike.  Unaweza kuamua sasa...

JINSI YA KUTENGENEZA BRAND IMARA

Image
Kila mtu anaweza kutengeneza BRAND imara kwa ajili ya taasisi, kampuni ama kikundi chake kwa kufanya yafuatayo:- 1. Sajili taasisi, kikundi, kampuni au biashara yako ili itambulike kisheria. 2. Tengeneza kanuni ambazo wafanyakazi ama wafuasi wako watazifuata. Kila mtu katika kutekeleza majukumu yake azifuate kanuni hizo. 3. Fanya kila linalowezekana kampuni, taasisi ama kikundi chako kiwe na uwezo wa kujiendesha hata usipokuwepo. Ukiona kikundi , kampuni ama taasisi yako bado haiwezi kujiendesha usipokuwepo jua kabisa hapo badooooo sanaaaa! 4. Tengeneza Logo, chapa t-shirts ili kutengeneza utambulisho wako kwa watu wanaokuzunguka.  Hii itasaidia watu kufahamu kikundi, kampuni ama taasisi yako pasipo kutumia nguvu kubwa. Sasa basi... Katika kufanikisha haya yoteeee..... Msomi Huru Enterprises Co. LTD inakusaidia kutengeneza brand imara sana kwa; ❇️ Kutengeneza logo, posters ama banners. ❇️ Kusajili kikundi, taasisi ama kampuni yako kwa gharama Nafuu sana (Kuna OFA ya msimu wa sikuku...

15 QUOTABLE QUOTES FROM THE BOOK 'PERMANENT SOLUTION TO YOUTH UNEMPLOYMENT'

Image
Author; Dr. Abib Olamitoye Analyst; Mr. Mashaka Siwingwa (CEO Msomi Huru Foundation) +255 764 987 588 01. "Do as I do is always better than do as I say." (Page 7-8) 02. "Whatever any man can accomplish, every other man also carries the capacity to do just as well." (Page 8) 03. "The stomach needs good food and the brain needs good books, for the man to function maximally." (Page 10) 04. "To make most of his God given potential, to exploit his talents to the peak, a man needs to feed the body daily and feed the brain daily." (Page 10) 05. "One of the fruits of the skill of saving is patience. You get to establish that the best way to get rich is to get rich slowly, and this is also the surest way to become rich with peace of mind." (Page 14) 06. "When the time to begin the business has come, the time to save up the capital has passed." (Page 15) 07. "There are basically two reasons why we set up a business, namely, to crea...

HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUJIEPUSHA NA MAMBO YASIYOFAA

Kwenye maisha tunaishi na watu tofauti tofauti na wenye mitazamo tofauti tofauti. Watu hao huweza kuwa na mitazamo mizuri ama mibaya juu ya mambo fulani. Mathalani, hata wewe kuna baadhi ya mambo ukiyaona unaweza kuyapambanua kama ni mazuri au mabaya. Wakati mwingine hutakiwi hata kusubiri kuambiwa kama jambo hilo ni jema ama baya. Ni mara nyingi sana (kama siyo zote) kwa marafiki hupeana au kupashana habari au taarifa fulani. Taarifa au habari hizo huhusu mambo yanayozizunguka jamii hizo. Wakati mwingine marafiki huweza kusambaza habari hizo na kutuletea bila kuzipima kwa kina na kuweza kuzichuja ili kujua kama zinafaa au la! Na wakati mwingine habari hizo huwa hazifai kabisa kusambazwa! Kosa letu kubwa ni pale ambapo tunaamua kusambaza taarifa au habari ambazo tumezipokea tu kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki zetu bila kuweza kuzipima wala kuzichuja ili kuweza kujua uhalali wa habari hizo. Ikiwa tumepokea taarifa au habari zisizoaminika kutoka kwa marafiki zetu moja kwa moja tunaten...

SIFA KUU YA MTU MWONGO

Ukiwa mtu mwongo ni raha sana kwa sababu ukidanganya mara ya kwanza utatamani udanganye tena na tena. Uongo ni mtamu kuliko ukweli na ni rahisi kuusema kwa sababu unavutia na kufariji kwa muda mfupi. Muhimu tu ni kwamba ukiwa mwongo unatakiwa baada ya kudanganya mara ya kwanza, ya pili na ya tatu uwe na kumbukumbu, ukumbuke mara zote ulizodanganya tena kwa mpangilio ule ule. Zaidi, uwe na uwezo wa kuwakumbuka uliowadanganya; hapo ndipo unapokuja kukamatwa kwa sababu uongo hauna sifa ya kudumu.  Watu hujisahau mara tu baada ya kudanganya na huwa hawana uwezo wa kukumbuka tena. Ndiyo maana hata kwenye sheria (mahakamani) watu hukamatwa na hatia mara baada ya kuchanganya maelezo ya awali na yale yaliyofuatia. Unakuta mtu baada ya kueleza sentensi A anashindwa kuiunganisha na sentensi B na C kwa sababu sentensi A haikuwa na ukweli. Hivyo, anakuwa na uwezekano mkubwa wa kuchanganya mambo na kukutwa na hatia. Ndugu yangu, ukweli unahitaji vithibitisho vingi na vielelezo vingi ili kuweza ...