TABIA KUMI RAHISI SANA ZA KUFANYA ILI UANZE KUFANIKIWA

Na; Mashaka Siwingwa

+255764987588

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Suala la kufanikiwa siyo tukio la sekunde moja au siku moja kama wengi wadhanivyo. Ni mchakato mrefu na wenye mfululizo wa matukio kadhaa. Hata hivyo, tulio wengi hatujui kanuni bora za kupitia ili tuweze kufanikiwa. Kwa kubeza ujumbe huu, kuna mdau anayeniona kila siku atasema mbona mimi sijafanikiwa! Shauri yako. 

Ili uweze kufanikiwa unahitaji vitu kadhaa muhimu sana. Hivi vitu vitaamua hatma ya maisha yako katika nyanja mbalimbali. 

Pasi na shaka, kuna mtu ataauliza kama kuna nyanja za maisha. Ndiyo, kuna nyanja mbalimbali za maisha. Kati ya hizo ni pamoja na kufanikiwa kiuchumi, kijamii, kisiasa, kiutamaduni na kadharika.

Baadhi ya tabia zifuatazo zinaweza kumtengenezea mtu mazingira ya kufanikiwa moja kwa moja. Au zinaweza kuwa mwanga wa mafanikio yake.

Kanuni au tabia hizo ni pamoja na;

1. Mtu anayezingatia kanuni za afya. Afya ni mtaji, kila mtu anapaswa kuiheshimu na kuzingatia kanuni za afya bora. Huweza kufanya shughuli za kiuchumi ukiwa unaumwa, huwezi kufanya siasa ukiwa na afya dhaifu. Hivyo, katika jua katika mvua, afya njema ni muhimu sana.

2. Mtu anayekula vizuri. Kula ni muhimu. Tena siyo kula tu, bali kula vizuri na kwa kuzingatia kanuni za lishe bora ikiwa ni pamoja na kupata mlo kamili.

3. Mtu anayefanya mazoezi. Siyo kujisumbua ni katika harakati za kuhakikisha kwamba unauweka mwili wako katika hali njema. Hii inakusaidia kuepukana na vitambi visivyo na ulazima wowote ule pamoja na mgando wa mafuta mwilini. Mazoezi ni muhimu sana kwa afya ya kila mmoja wetu.

4. Mtu anayechunguza afya yake mara kwa mara. Fanya mazoezi, pima afya mara kwa mara. Wakati mwingine inatokea unakuta mtu anaumwa leo lakini kumbe hayo maradhi yalianza miezi miwili kabla. Kwa hiyo, ni vema kama ukijijengea tabia ya kucheki afya yako mara kwa mara. Tatizo sisi wabongo kama mtu hajapata tatizo la kulazwa humuoni kwenye vituo vya afya. Huko kumekuwa bangi na kituo cha polisi.

5. Mtu mwenye kiasi kwenye suala la starehe. Starehe zinapita; Acha zikupite. Kama wewe siyo wa ukanda wa pwani siyo lazima uhudhurie kila birthday, pangilia matumizi yako vizuri. Epuka gharama za maisha zisizo na maana.

6. Mtu anayepata ushauri mzuri wa masuala ya fedha. Angalia watu wazuri katika masuala ya fedha na uchumi. Upate ushauri hata kabla hujaanza matumizi. Kamwe usitumie kabla ya kupanga bajeti yako. Hii itakusaidia sana kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima.

7. Mtu anayesoma vitabu. Soma sana mpaka makaratasi yakuogope. Soma mpaka ifikie wakati usahau vitabu kwenye mto wako wa kulalia. Yapo mambo mengi sana huko kwenye vitabu. Endelea kuviona kituo cha polisi sasa.

8. Mtu anayewekeza vizuri. Siyo tu fedha, hata mawazo yako jitahidi uyawekeze kwenye vitu chanya.

9. Mtu anayedhibiti matumizi yake. Tumia kistaarabu. Pangilia bajeti zako vizuri.

10. Mtu anayemtanguliza Mungu kwenye kila jambo. Mungu awe ndiyo kila kitu kwako. Kabla hujafanya chochote kile mshirikishe Mungu wako. Vyote vilivyotajwa hapo juu si kitu kabisa kama hutofanya ukiwa na Mungu. Tafuta sana kuwa na unyoofu wa moyo mbele za mwenyezi Mungu.

msonihurublog.blogspot.com


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

KWA NINI WATU WENGI HAWANA UTAMADUNI WA KUJISOMEA VITABU?

Mbwa Bado Hajafa! (Usikubali Kukata Tamaa)

KAULI KUMI ZA HAYATI MWL. JULIUS K. NYERERE KUHUSU ELIMU NDANI NA NJE YA NCHI