Posts

Fahamu Kwa nini Unapaswa Kujenga Tabia ya Kujisomea Vitabu (Faida za Kujisomea Vitabu)

Image
(Sehemu ya Pili) Habari... Mara ya mwisho tuliangazia sehemu ya kwanza ya somo hili ambapo tuliangalia kwa utondoti sababu za kwa nini watu hawapendi/hawana utamaduni wa kujisomea vitabu. Moja ya sababu ambayo tuliangalia ni watu kutojua umuhimu wa kujisomea vitabu.   Basi leo katika sehemu hii natamani tujue faida za kusoma vitabu pengine tunaweza kuwaamsha baadhi ya wenzetu na kuwatia hamu ya kusoma. Zifuatazo ni faida za kujisomea vitabu; >> Kuongeza Maarifa: Vitabu ni chanzo kikuu cha maarifa na taarifa. Kusoma vitabu kunakuwezesha kujifunza mambo mapya na kuongeza uelewa wako wa ulimwengu. >> Kuboresha Uwezo wa Kufikiria: Kusoma vitabu kunachochea ubongo kufanya kazi, hivyo kuboresha uwezo wako wa kufikiria kwa undani, kutatua matatizo, na kufanya maamuzi bora. >> Kuboresha Lugha na Msamiati: Kusoma vitabu husaidia kuboresha uwezo wa lugha, kuongeza msamiati, na kuelewa matumizi sahihi ya maneno. >> Kuongeza Uwezo wa Kujieleza: Kusoma vitabu kunasaidia ...

KWA NINI WATU WENGI HAWANA UTAMADUNI WA KUJISOMEA VITABU?

Image
 Kwa Nini Watu Wengi Hawana Utamaduni/Hawapendi Kujisomea Vitabu?  (Sehemu ya Kwanza) Habari... Siku kadhaa zilizopita niliandika kwenye kurasa zangu za mitandao ya kijamii mara baada ya kufanya kipindi cha 'The Fix' cha redio kuhusiana na mada inayosema 'Kwa Nini Watu Wengi Hawapendi Kusoma Vitabu?' Nakumbuka baada ya chapisho lile niliahidi kukufikishia somo lote hatua kwa hatu. Sasa leo natamani somo hili liwe kama sehemu ya kwanza na mada ile ile ambapo leo tutaangalia sababu za watu wengi kutokuwa na mwamko, shauku ama utamaduni wa kujisomea vitabu. Zifuatazo ni baadhi tu ya sababu za watu wengi kutokuwa na utamaduni wa kujisomea vitabu; >> Mabadiliko ya Teknolojia (Simu na Mitandao ya Kijamii); Vifaa vya kisasa kama simu za mkononi, kompyuta, na mitandao ya kijamii vimechukua nafasi kubwa katika maisha ya watu. Watu wengi wanapendelea kutumia muda wao kwenye mitandao badala ya kusoma vitabu. >> Video na Habari za Papo kwa Papo; Watu wanaweza kupata hab...

Mbwa Bado Hajafa! (Usikubali Kukata Tamaa)

Image
Meshack Siwingwa 0764 987 588 Jamaa mmoja alikuwa akisafiri kutoka nyumbani kwake kuelekea mjini majira ya saa moja asubuhi. Baada ya mwendo wa kama saa mbili hivi alikutana na kijana mmoja akiwa amesimama barabarani akingojea kumwona mtu aendaye mjini ili aweze kumuomba 'lift.' Kijana huyu alikuwa amebeba vifaa kadhaa vinavyotumika kwa ajili ya usafi wa kuoshea magari vile ambavyo alivimudu kuvibeba. Kando ya huyu kijana alikuwa amelala mbwa aliyeonekana kuwa dhooofu bin hal kwani alikuwa akitweta kwa uchungu uliosababishwa na maumivu aliyokuwa nayo. Yule kijana alipunga mkono kwa jamaa ndipo jamaa aliposimamisha gari yake na kuamua kumsikiliza kijana. Kijana alimweleza jamaa kwamba alikuwa anaelekea mjini kumtibia mbwa wake na kwamba baadhi ya vifaa kadha alivyokuwa navyo alitegemea apate kazi za kuosha magari pindi afikapo mjini ili aweze kupata fedha za kumudu gharama za matibabu ya mbwa wake. Jamaa alishangaa sana baada ya kuona hali ya mbwa wa yule kijana na ndipo alipoam...

SABABU KUBWA (06) KWA NINI WAFANYABIASHARA 'WANAOJITAMBUA' WANATUMIA BUSINESS CARDS

Image
 Yes, unaweza kuonekana ni mtindo mgeni wa maisha lakini hii ni moja kati ya njia rahisi sana za kufanya marketing ya biashara au huduma yako. Matumizi ya business cards katika kutangaza biashara au huduma yako yana faida kadhaa kubwa sana.  Hapa chini ni faida chache tu! Mosi, business cards huonesha smartness kwenye ufanyaji wa biashara au utoaji wa huduma yako. Mtu yeyote yule anapokuomba mawasiliano yako ukampatia business cards; moja kwa moja anajua kwamba upo serious na unajua vyema unachokifanya. Pili, business cards hujenga uaminifu. Wateja wengi hukuamini wewe pamoja na huduma au biashara yako hasa mara baada ya kujiridhisha kwamba uko formal sana.  Tatu, huongeza ujasiri. Unapotumia business cards kuendesha huduma au biashara yako, hii inakuongezea ujasiri hata wewe mwenyewe hasa pale ambapo mtu anakuomba contacts unampatia business cards 😎 Nne, ni njia mojawapo ya kutangaza biashara au huduma unayofanya. Tuchukulie mfano umekutana na ndugu ambaye muda mrefu ha...

Je, Huyu ni Wewe?

Image
Je, unahitaji kudesign na kuprinti stickers? Je, unahitaji kudesign na kuprinti vitabu vya tickets? Je, unahitaji kudesign na kuprinti ID Cards? Je, unahitaji kuprinti t-shirts? Je, unahitaji kudesign na kuprinti vitabu vya risiti (receipt books)? Je, unahitaji kudesign na kuprinti flyers? Je, unahitaji kudesign na kuprinti business cards? Je, unahitaji kudesign na kuprinti vitabu vya malipo (payment vouchers)? Wala Usipate Shida... ... Msomi Huru Enterprises Co. LTD ndiyo jibu lako! Tunafanya designing za ubora wa hali ya juu pamoja na printing aina zote (zenye viwango vya TBS) Tunakukaribisha sana kufanya kazi na sisi na kwa hakika, HAUTAJUTA KUTUAMINI📌 Wasiliana nasi kwa simu namba: 0764 987 588 Barua pepe:  msomihurugroup@gmail.com Tupo Mzumbe - Morogoro Karibuni Sana!

HIZI HAPA SABABU 100+ KWA NINI UNATAKIWA UKUZE BRAND YAKO KWANZA NDIPOSA UONE MAFANIKIO YAKITIRIRIKA KAMA MAJI YA MTO YORDANI!

Image
  Watu wengi sana ambao ni wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali huwa wanajikuta wakiwa kwenye mkanganyiko mkubwa mkubwa sana wa kipi wanachotakiwa kufanya kati ya kukuza brand zao kwanza ama kuendelea kutoa huduma tu. Wengine hukaribia hata kiasi cha kukata tamaa hasa pale wanapokuwa hawaoni matokeo ya kile wanachokifanya. Ukweli ni kwamba, ni muhimu sana kukuza brand yako wakati unaendelea kutoa huduma ama kufanya biashara zako ili watu waweze kukuamini na kufanya kazi na wewe ama kununua kutoka kwako. Hii inasaidia kiasi kwamba unafika wakati ambapo wateja wakiwa na uhitaji mbalimbali lazima waje kununua kutoka kwako kwa sababu ya brand yako. Wakati mwingine kinachokusaidia kuuza au kupata wadau siyo aina ya bidhaa zako unazotoa, bali ni kwa sababu ya brand au jina lako linavyofahamika. Habari njema ni kwamba, hata wewe unayonafasi kubwa sana ya kupambania brand yako wakati unaendelea kufanya biashara yako. Brand itakutangaza na kukufanya uaminike.  Unaweza kuamua sasa...

JINSI YA KUTENGENEZA BRAND IMARA

Image
Kila mtu anaweza kutengeneza BRAND imara kwa ajili ya taasisi, kampuni ama kikundi chake kwa kufanya yafuatayo:- 1. Sajili taasisi, kikundi, kampuni au biashara yako ili itambulike kisheria. 2. Tengeneza kanuni ambazo wafanyakazi ama wafuasi wako watazifuata. Kila mtu katika kutekeleza majukumu yake azifuate kanuni hizo. 3. Fanya kila linalowezekana kampuni, taasisi ama kikundi chako kiwe na uwezo wa kujiendesha hata usipokuwepo. Ukiona kikundi , kampuni ama taasisi yako bado haiwezi kujiendesha usipokuwepo jua kabisa hapo badooooo sanaaaa! 4. Tengeneza Logo, chapa t-shirts ili kutengeneza utambulisho wako kwa watu wanaokuzunguka.  Hii itasaidia watu kufahamu kikundi, kampuni ama taasisi yako pasipo kutumia nguvu kubwa. Sasa basi... Katika kufanikisha haya yoteeee..... Msomi Huru Enterprises Co. LTD inakusaidia kutengeneza brand imara sana kwa; ❇️ Kutengeneza logo, posters ama banners. ❇️ Kusajili kikundi, taasisi ama kampuni yako kwa gharama Nafuu sana (Kuna OFA ya msimu wa sikuku...