UKITAKA WATU WAKUHESHIMU FANYA HIVI
Kila mtu anastahili kupewa heshima na kuthaminiwa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba heshima na thamani ni kitu ambacho kila mtu anastahili. Haijalishi elimu zetu, tamaduni zetu, makabila yetu, dini zetu wala maeneo tunayotokea. Kutokuheshimiana ni moja ya kitu ambacho kimekuwa kikisababisha migogoro kwa watu mbalimbali. Mtu mmoja anaposhindwa kumheshimu mwenzake hupelekea migogoro na hata kuvunja ukaribu wao. Marafiki wawili wanaposhindwa kuheshimiana huwa hawana haja tena ya kuona kama urafiki wao una manufaa yoyote yale bali huamua kuvunja urafiki wao. Wapenzi wengi pia wanaposhindwa kuheshimiana hupelekea mogogoro kwenye mapenzi yao na hata kuvunja mahusiano. Mathalani, wanandoa wanaposhindwa kuheshimiana na kuthaminiana hupelekea migogoro ndani ya nyumba na hatimaye kuamua kuvunja mahusiano au ndoa yao. Kwa kawaida, suala la kutoheshimiana ni suala la mtu mmoja mmoja kwani ni matokeo ya ubinafsi baina yetu. Kwa mujibu wa Dkt. Issaya Lupogo & Aziza Lupogo (2019) katika kita...