Fahamu Kwa nini Unapaswa Kujenga Tabia ya Kujisomea Vitabu (Faida za Kujisomea Vitabu)

(Sehemu ya Pili) Habari... Mara ya mwisho tuliangazia sehemu ya kwanza ya somo hili ambapo tuliangalia kwa utondoti sababu za kwa nini watu hawapendi/hawana utamaduni wa kujisomea vitabu. Moja ya sababu ambayo tuliangalia ni watu kutojua umuhimu wa kujisomea vitabu. Basi leo katika sehemu hii natamani tujue faida za kusoma vitabu pengine tunaweza kuwaamsha baadhi ya wenzetu na kuwatia hamu ya kusoma. Zifuatazo ni faida za kujisomea vitabu; >> Kuongeza Maarifa: Vitabu ni chanzo kikuu cha maarifa na taarifa. Kusoma vitabu kunakuwezesha kujifunza mambo mapya na kuongeza uelewa wako wa ulimwengu. >> Kuboresha Uwezo wa Kufikiria: Kusoma vitabu kunachochea ubongo kufanya kazi, hivyo kuboresha uwezo wako wa kufikiria kwa undani, kutatua matatizo, na kufanya maamuzi bora. >> Kuboresha Lugha na Msamiati: Kusoma vitabu husaidia kuboresha uwezo wa lugha, kuongeza msamiati, na kuelewa matumizi sahihi ya maneno. >> Kuongeza Uwezo wa Kujieleza: Kusoma vitabu kunasaidia ...