SABABU KUBWA (06) KWA NINI WAFANYABIASHARA 'WANAOJITAMBUA' WANATUMIA BUSINESS CARDS

Yes, unaweza kuonekana ni mtindo mgeni wa maisha lakini hii ni moja kati ya njia rahisi sana za kufanya marketing ya biashara au huduma yako. Matumizi ya business cards katika kutangaza biashara au huduma yako yana faida kadhaa kubwa sana. Hapa chini ni faida chache tu! Mosi, business cards huonesha smartness kwenye ufanyaji wa biashara au utoaji wa huduma yako. Mtu yeyote yule anapokuomba mawasiliano yako ukampatia business cards; moja kwa moja anajua kwamba upo serious na unajua vyema unachokifanya. Pili, business cards hujenga uaminifu. Wateja wengi hukuamini wewe pamoja na huduma au biashara yako hasa mara baada ya kujiridhisha kwamba uko formal sana. Tatu, huongeza ujasiri. Unapotumia business cards kuendesha huduma au biashara yako, hii inakuongezea ujasiri hata wewe mwenyewe hasa pale ambapo mtu anakuomba contacts unampatia business cards 😎 Nne, ni njia mojawapo ya kutangaza biashara au huduma unayofanya. Tuchukulie mfano umekutana na ndugu ambaye muda mrefu ha...