HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUJIEPUSHA NA MAMBO YASIYOFAA
Kwenye maisha tunaishi na watu tofauti tofauti na wenye mitazamo tofauti tofauti. Watu hao huweza kuwa na mitazamo mizuri ama mibaya juu ya mambo fulani. Mathalani, hata wewe kuna baadhi ya mambo ukiyaona unaweza kuyapambanua kama ni mazuri au mabaya. Wakati mwingine hutakiwi hata kusubiri kuambiwa kama jambo hilo ni jema ama baya. Ni mara nyingi sana (kama siyo zote) kwa marafiki hupeana au kupashana habari au taarifa fulani. Taarifa au habari hizo huhusu mambo yanayozizunguka jamii hizo. Wakati mwingine marafiki huweza kusambaza habari hizo na kutuletea bila kuzipima kwa kina na kuweza kuzichuja ili kujua kama zinafaa au la! Na wakati mwingine habari hizo huwa hazifai kabisa kusambazwa! Kosa letu kubwa ni pale ambapo tunaamua kusambaza taarifa au habari ambazo tumezipokea tu kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki zetu bila kuweza kuzipima wala kuzichuja ili kuweza kujua uhalali wa habari hizo. Ikiwa tumepokea taarifa au habari zisizoaminika kutoka kwa marafiki zetu moja kwa moja tunaten...