HIVI NDIVYO TUNAVYOWEZA KUSAPOTI WAHITIMU WAPYA KUANZISHA BIASHARA
Na:- Mashaka Siwingwa +255764987588 ____________________________________________________________________________________ Mnamo Juni 2021, niliweza kupokea kadi za aina tatu tofauti tofauti. Ninaweza kusema kwamba ulikuwa ni mwezi wa neema sana kwangu kiasi kwamba nilithaminiwa mpaka kufikia hatua ya kupewa kadi. Kadi ya kwanza ilikuwa imenakshiwa safi kabisa kwa rangi ya mzambarau. Ilikuwa ni kadi nzuri na yenye kuvuti. Ilikuwa ni kadi iliyoambatanishwa na jina langu kabisa tena kwa herufi kubwa. Baada ya kuifungua na kuisoma ilikuwa ikinitaka kuchangia harusi ya rafiki yangu ambaye alitarajia kufunga pingu za maisha Oktoba, 2021. Nilimshukuru sana Mungu kwa kitendo cha mimi kuonekana wa maana mpaka kufikia hatua ya kupewa kadi ya kuchangia harusi. Hiyo niliiweka chini. Baada ya kuiweka chini niliichukua kadi ya pili. Hii ilionekana kuwa ya hadhi ya chini kidogo na haikupambwa sana kama ile ya awali. Niliipokea kutoka kwa rafiki yangu wa karibu. Nilivyoifungua na kuisoma niligundua kwa...