KAULI KUMI ZA HAYATI MWL. JULIUS K. NYERERE KUHUSU ELIMU NDANI NA NJE YA NCHI
Na; Mashaka Siwingwa +255764987588 ----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------- Ni miaka mingi imepita tangu atutoke baba wa taifa Hayati, Julius Kambarage Nyerere. Ushujaa na uhodari wake katika kupambanua mambo pamoja na kueleza vitu bayana kunamfanya aendelee kuwa shujaa asiyesahaulika. Wakati wa uhai wake, baba wa taifa alisisitiza sana juu ya suala la elimu hapa nchini. Falsafa yake ya kuamini kwamba elimu ndiyo silaha pekee ya kuufikia ukombozi wa kweli hasa kifikra. Katika nyakati tofauti tofauti, katika sehemu tofauti na katika muktadha tofauti, Hayati baba wa taifa aliweza kuonesha wazi msimamo wake juu ya mfumo wetu wa elimu. Kati ya mengi aliyoyazungumza, leo nimeamua nikukusanyie kauli kumi tu alizowahi kuzitoa shujaa huyu. Twende sawa; 1. Kauli aliyoitamka mnamo tarehe 31 Desemba, 1969 akizungumza na vyombo vya habari kuhusu malengo ya Elimu ya Watu Wazima. Alisema, "... education is som...