TANZANIA NA FURAHA YA MNYONGE ISIYODUMU KAMWE
Kifo cha Hayati Dkt. John P. Magufuli, kimewaacha wanyonge wengi sana wakilia bila kuona suluhu. Mpaka sasa bado kuna watanzania pamoja na waafrika kwa ujumla, wengi sana ambao bado hawaamini kama kweli jemedari wetu ametutoka! Aghalabu sasa hivi wameanza kuamini. Ni sahihi kabisa kwamba kifo cha mpendwa wetu huyu ni pengo lisilozibika kamwe, hili halipingiki. Lakini watu wengi sana wamekuwa wakimhusisha jemedari Magufuli na Musa wa Israeli aliyefanyika mkombozi wa taifa lake kwa kuwatoa wenzake misri na kuwapeleka katika taifa la ahadi. Hata hivyo, ndoto ya Musa haikutimia kama alivyodhani. Sasa tujiulize kidogo, kwanini Magufuli kama Musa? Kwa nini, si mwingine? Kwa nini asifananishwe na Sauli? Suleimani na wengine wote? Hebu pitia andiko hili lililoandaliwa na kijana mahiri sana katika uga wa uandishi na ninaamini halitakuacha mtupu; hakika lazima utapata cha kujifunza. Twende sawa sasa. Wana wa Israel walilia sana na walishindwa hata kukubali kifo cha Musa. Ungewaambia n...